NA DENIS MLOWE IRINGA
KATIKA kuhakikisha ushindi wa kishindo kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Iringa imefanya mafunzo maalum kwa makatibu wenezi wa kata 28 zilizoko katika wilaya hiyo.
Mafunzo hayo yameongozwa katika ilani ya chama hicho 2025-2030 yenye vipaumbele ambavyo makatibu wenezi wa wilaya hiyo kutumia katika kukinadi chama cha mapinduzi kwa wananchi yenye kuwaletea maendeleo chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kuweza kuibuka na ushindi.
Akizungumza katika mafunzo hayo Katibu wa Sasa na Uenezi wilaya ya Iringa Vjijini Anold Mvamba alisema Ilani ya uchaguzi inawahusu wanachama na viongozi wa CCM hivyo wanaumuhimu mkubwa wa kuisoma na kuelewa pindi wakienda kwa wananchi watoe elimu faida ya ilani hiyo katika kuelekea maendeleo ya wananchi kwa ujumla kutokana na ubora wake.
Mvamva alisema kuwa mafunzo hayo kwa wenezi yamefanyika kwa kuwa ilani hiyo waisome na kuielewa vizuri kwani imegusa nyanja mbalimbali ikiwemo sekta ya Kilimo, Afya,Elimu,Nishati.
“Naomba sana mkasome ilani hii iwafikie wananchi na kujipa ushindi wa kishindo chama cha mapinduzi CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa October 2025 kwani chama cha mapinduzi chini ya Mwenyekiti wake Taifa Rais Samia mambo makubwa yamefanyika kwa miaka michache tangu aliposhika serikali na kuwaletea maendeleo wananchi na ilani hii ni funga kazi.” Alisema
Naye Katibu wa CCM wilaya ya Iringa vijijini Sure Mwasanguti alisema makatibu wenezi wanapaswa kufahamu katiba ya chama na maelekezo ya chama hasa katika kuelekea uchaguzi mkuu huku akiwakumbusha kutimiza wajibu wao na kuhakikisha chama cha Mapinduzi kinashinda kwa kishindo kwani ilani imetekelezwa vizuri na ilani ya 2025-2030 imejielekeza kutatua changamoto za wananchi.
Mgeni wa heshima katika mafunzo hayo Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa vijiji Ndugu Constantino Kihwele amewataka wenezi hao kutambua nafasi zao na kutobeba wagombea kwani
chama kinakwenda kupata wagombea wenye sifa ambao watapeperusha bendera ya CCM katika nafasi zote.
Kihwele amewataka wenezi hao kueleza mambo ya maendeleo yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita huku akiahidi kura za kishindo kwa wagombea wote wa CCM kwani kazi iliyofanywa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Samia yatapeperusha bendera ya CCM kwa kura za kishindo.
Baadhi ya wenezi walisema kuwa watahakikisha ilani hiyo inasambazwa kwa nguvu zote kwa wananchi waelewe kwani imewagusa wananchi wa matabaka yote na vipaumbele vinavyogusa wananchi.
Aidha wamepongeza uongozi wa wilaya kwa kuwapatia mafunzo ambayo yataleta chachu katika kuleta ufahamu, nia na malengo ya CCM katika kuwaletea vipaumbele wananchi kupitia ilani ya 2025- 2030.