Na Ahmed Mahmoud Arusha
Katibu Mkuu wa wizara ya Elimu sayansi na teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo amevitaka vyuo ya ualimu 35 nchini kuvituza vifaa na vitabu walivyopewa kutoka serikali ya Canada ili kusaidia kuongeza ubora wa elimu nchini.
Dkt.Akwilapo Aliyasema hayo wakati akikabidhi vifaa na vitabu vya kufundishia na kujifundishia waalimu ikiwa ni sehemu ya mradi wa kuendeleza elimu ya ualimu TESP wenye thamani ya zaidi ya bilion 90 kwenye hafla iliyofanyika jijini Arusha.
Alisema kuwa msingi na uboreshaji elimu nchini unaanzia kwenye ufundishaji wa wanafunzi hivyo fedha na vifaa hivyo vimekuja wakati muafaka kwa lengo kuu la kuboresha elimu.
Akaeleza kuwa lengo kuu la mradi huo wa kuendeleza elimu ya ualimu ni kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa waalimu nchini ili kukuza viwango vya elimu zao kwenye ufundishaji wanafunzi nchini.
“Ni mategemeo ya serikali kuona vifaa hivi vikituzwa kuweza kusaidia vizazi vijavyo kuhakikisha uboreshaji wa elimu nchini huku akiwataka wakuu wa vyuo kuona umuhimu huo na kusimamia kwa faida ya kuongeza tija katika ufundishaji” alisisitiza Dkt.Akwilapo
Awali akiongea kwenye hafla hiyo Gwen Walmsley alirudia kuipongeza Tanzania kwa juhudi zake za uboreshaji wa elimu na nchi hiyo itaendeleza ushirikiano kwenye sekta hiyo ili kuweza kuongeza na kuboresha ufundishaji wa wanafunzi.
Alisema kuwa wamefurahi kuona mradi huo ukisaidia kuongeza tija kwenye ufundishaji kwa waalimu kupata vifaa hivyo kwenye vyuo vya ualimu nchini na kuwataka waalimu kuendelea kutumia vifaa hivyo kuongeza maarifa kuendana na teknolojia ya Tehama duniani.
Serikali ya Canada imetoa jumla ya kompyuta 780 kompyuta mpakato 43 mashine za kudurufu (printers) 74 vitabu 26,470 Photocopy mashines 35 projectors 100 na dijiti duplicators 35 .
Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa kwa chuo cha Elimu Maalum ya ualimu Patandi kwa niaba ya vyuo vya ualimu 35 vya serikali ambapo mkuu wa chuo hicho Lucian Segesela alishukuru kwa niaba yao na kuahidi kuvitunza vifaa hivyo.
Alisema kuwa vifaa hivyo vimekuja wakati muafaka na vitasaidia kuongeza uboreshaji wa elimu nchini na kwa waaalimu tarajali kuongeza ufanisi wa ufundishaji na kujifunza kwa tija.
Nae Rais wa wanafunzi wa chuo hicho Engrebert Alex aliishukuru serikali zote mbili na kueleza kwamba Sasa wanaenda kuvitumia vifaa hivyo kuboresha mazingira ya ufundishaji kwa wanafunzi nchini.