Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo,CPA Pius Maneno akifungua warsha hiyo jijini Arusha.


Washiriki wakifuatilia mada mbalimbali katika warsha hiyo ya siku nne jijini Arusha.
Happy Lazaro,Arusha
BODI ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa hesabu Tanzania (NBAA) imewakutanisha Wahasibu na Wakaguzi wa Taasisi na kampuni binafsi zaidi ya 150 kutoka maeneo mbalimbali wamekutana jijini Arusha katika warsha ya siku nne yenye lengo la kuwajengea uwezo katika maswala mbalimbali .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha mara baada ya kufungua warsha hiyo,Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo,CPA Pius Maneno amesema kuwa ,lengo kuu la warsha hiyo ni kuwasaidia wahasibu kuandaa taarifa za fedha za mwaka kwa kutumia viwango vya kimataifa vya uandaaji wa hesabu za serikali IPSAS).
CPA Maneno amesema kuwa wamekuja Arusha kwa ajili ya warsha ya siku nne kuongelea viwango vya kimataifa vya utayarishaji wa hesabu za mashirika,Taasisi ,serikali kwa ujumla hesabu za umma .
“Wanafanyaja hivyo kwa sababu hivi ni viwango vya utayarishaji wa hesabu ambavyo vimekuwa vinatumika Tanzania kuanzia June 30,2013 na baadaye Sheria ikabadilishwa ikawa ya 2015 ikawekwa kwenye Sheria ya fedha za umma .”amesema .
Amesema kuwa sababu ya kufanya hivyo ni kuwa wahasibu au wakaguzi wanabadilika na wanakuja wengine na wengine wanastaafu wanaondoka hao wanakuja vijana na hawavijui viwango hivi ,hivyo inabidi viwango hivi waendelee kufundisha kila wakati .
“Tunamtaka mhasibu aliyehitimu angalau ahudhurie masaa 30 kwa mwaka na mwasibu aliyebobea msaa 40 kwa sababu viwango hivi vya hesabu vinabadilika vyote ikiwemo vya umma ama binafsi vinabadilika .”amesema CPA Maneno.
Amesema kuwa ,kupitia warsha hiyo wanakumbushana hivyo viwango vinatumika namna gani na kuangalia vya zamani vinatumika namna gani na vipya vinavyokuja .
“Hapa tunao wahasibu na wakaguzi na wengine wenye kutaka kusikiliza na wadau zaidi ya 185 ambao wamehudhuria hii hapa kwa siku nne .”amesema .
Ameongeza kuwa, wanajifunza mambo mbalimbali namna gani watunze mali za umma ,namna gani wakusanye mapato na wanapokusanya wanaweka namna gani na kufanya yaonekane vizuri ili mtu mwingine ambaye sio mwasibu au mkaguzi ajue hapo wanakusanya shs ngapi .
“Wanafundishwa pia utunzaji wa daftari la hesabu kwamba mali ziwepo na hesabu za fedha ziwepo na mwisho wa siku waangalie ni vitu gani ambavyo kwa nchi yetu katika mazingira yetu havipo vizuri sana na kwamba virekebishwe ili washauri viwango vibadilishwe “amesema .
“Tumekuwa tukifanya hivi kila mwaka zaidi ya mara nne kuhusu utayarishaji wa hesabu za fedha za umma na nyingine wanafanya kila mwezi wana semina moja ila hii ya leo ni warsha mtu anatakiwa aelewa asilimia 75 pale pale na semina aelewe kwa asilimia 25 ya hivyo vinatosha ila ya leo tunaonyesha na mifano na nini cha kufanya ili mtu aelewe kwa asilimia 75 ili akitoka hapa ameiva .”
Kwa upande wake mshiriki wa warsha hiyo amesema kuwa, mafunzo hayo yanayotolewa na NBAA imeandaliwa huku lengo kubwa likiwa ni namna ya kuandaa financial statement kwa kutumia viwango vya kimataifa vya Wahasibu.
Amesema kuwa, wamejifunza mabadiliko mbalimbali ambayo yanatokea katika hivyo viwango ambavyo wanavitumia katika kuandaa vitabu vyao kama wanavyofahamu huu ni mwezi June ambapo kama serikali ni mwisho wa mwaka wa fedha na baada ya juni 30 wanahitajika kuaandaa vitabu vya mwaka 2024/2025.
Amesema kuwa, warsha hiyo pia ina malengo ya kuwakumbusha wahasibu kuhusu vile viwango mbalimbali ambazo nyingine ni mpya na kuweza kujua kuwa kuna vitu vinaenda kubadilika kwenye kuandaa financial statement zingine za mwaka unaofuata .
“Warsha hii itatusaidia kuandaa financial statement kulingana na viwango vya kimataifa vinavyotakiwa na kulingana na mabadiliko kama tunavyofahamu kuna mabadiliko mengi sana sasa hivi ambayo yanaendelea katika tasnia yetu ya uhasibu kwa hiyo imekuja kwa wakati kwani ni kipindi ambacho tunaenda kuandaa vitabu vyetu kulingana na viwango vinavyohitajika.”amesema .