TAARIFA KWA WATEJA WETU WA JIJI LA DODOMA
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawaomba radhi Wateja wake wa Jiji la Dodoma kwa katizo la umeme likilotokea leo Februari 10, 2020 saa 12:00 jioni.
Sababu Hitlafu imetokea kwenye “Cable Incomer” inayopeleka umeme “Zuzu Power Station” na kusababisha baadhi ya laini kukosa umeme.
Maeneo yanayoathirika ni:- Nkuhungu, Ndachi, Kizota, Four ways, Kikuyu, Chinangali, Chang’ombe, Hazina,Iringa road, Magorofa mengi, Mlowa, Mpunguzi, Matumbulu, Mvumi, Ntyuka, Chinyoya na baadhi ya maeneo ya wilaya ya Bahi na Chamwino.
Wataalamu wetu na mafundi wanafanya jitihada ili huduma irejee mapema.
Tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza
Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100
Tovuti: www.tanesco.co.tz,
Mitandao ya kijamii
Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,
Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetultd/
Instagram: tanesco_official_page
Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu