Sehemu ya walimu na wanafunzi wakichukua dondoo wakati wa warsha hiyo |
Wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa rsha hiyo |
WANANCHI wa Mkoa wa Tanga ambao wamekuwa na tabia za kutoku huisha maeneo ya
ardhi wanayomiliki kihalali baada ya kupita miaka 35 wamepewa tahadhari kwamba
wanaweza kujikuta wakipoteza sifa za kuendelea kuwa wamiliki kwa mujibu wa
sheria.
Kwani hatua hiyo inatokana na kwamba asilimia kubwa baada ya kupata umiliki
wa ardhi wanashindwa kutambua kwamba kila baada ya miaka hiyo kupitia wanapaswa
kwenda kuyahuisha kisheria badala yake wamekuwa wakiendelea kumiliki.
Hayo yalisemwa na Afisa Sheria wa Chama cha Wanasheria Wanawake
Tanzania (TAWLA) Mkoani Tanga Mwanaidi Kombo wakati wa warsha ya klabu za ardhi
kwa shule za sekondari na Kilulu na Magila iliyohusisha wanafunzi nane kila
shule na walimu wawili na kufiia jumla yao washiriki ishirini.
Klabu hizo zimeanzishwa kwenye shule hizo kupitia mradi wao wa kuwezesha
upatikanaji wa haki za wanawake katika kumiliki, kupata, kutumia na kufanya
maamuzi juu ya ardhi na mali jambo ambalo litawawezesha kuwasaidia kuondoa
vikwazo kwenye jamii.
Alisema kutokana na uzoefu uliopo unaonyesha kwamba watu wengi hawahuishi
umiliki wa wa ardhi baada ya kupitia miaka thelathini na tano kwa sababu
wanajiona ni wamiliki tu .
“Uhalisia ardhi inapofikisha miaka 35 baada ya hapo unatakiwa
kuihusisha tena kwani kuna hatari unaweza kunyang’anywa lakini pia uangalie
miliki yako ni kubwa au ni ndogo kwani leo serikali inaweza kutangaza watu
waliofikisha miaka 35 bila kuhuisha maeneo yao yanachukuliwa na kuuzwa”Alisema
Afisa Sheria huyo.
“Asilimia kubwa ya watu wa Tanga wamekuwa hawahuishi maeneo yao baada
kupitia miaka inayotakiwa kufanya hivyo hii ni changamoto ikipita miaka 35 bila
kuhuisha unakuwa unakosa haki kisheria kumiliki eneo husika”Alisema.
Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi kwamba lazima watazame hati
miliki yao ni aina gani ni kubwa au ni ndogo kama imefikia ukomo au bado lakini
kama imefika ukomo waende wakaihuisha kwani iwapo serikali ikisema watu ambao
wameshindwa kuihuisha maeneo yao wanachukua ni kweli wanachukua na ni haki yao
kisheria.
Awali akizungumza Mratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA)
mkoani Tanga Wakili Latifa Mwabondo uanzishwaji wa klabu hizo utasaidia
kupunguza changamoto zilizopo kwenye jamii kutokana na baadhi yao kutokuwa na
elimu ya kutosha kuhusiana na masuala la ardhi
“Tumeona tutilie mkazo masuala ya elimu mtu anapojua ni rahisi kuweza
kukipata na sehemu nyingi walipokuwa wakifanya midahalo imewapa uelewa jamii
kuhusu umuhimu wa kupata haki zao”Alisema
Aidha alisema wanawapatia elimu ili waweze kuisambaza kwa wenzao na kuweza
kuiendelezaa kwenye klabu zao za mashuleni zinazohusiana na ardhi jambo ambalo
litawasaidia kuipa uelewa jamii kuhusiana na changamoto za ardhi
zinapojitokweza kwenye maeneo yao.
Hata hivyo alisema wakiwapa elimu hao wakiwa na umri mdogo watakuwa waelewa
na kuweza kujitetea na kuweza kutoa elimu kwenye jamii ikiwemo kuwa mabalozi
wazuri kuilemisha jamii na kuwa mabalozi wa kutangaza Tawla.
Akieleza sababu za kuendesha mradi huo wilayani humo, Wakili Latifa alisema
kwamba Muheza ikiwa ni wilaya yenye wawekezaji wengi na makabila ikiwemo
wabondei ambao wanaamini sana mfumo dume.
Alisema kwamba mfumo huo umekuwa hautoi haki sawa kwa mwanamke kwenye
kumiliki ardhi ya urithi jambo ambalo limepelekea asilimia kubwa ya wao
kuwakosesha haki kuhusiana na haki zao wao hivyo wanachofanya ni kutetea sheria
kueielekeza sheria inayosema na sio kufanya watu wagombane.
“Katiba inatambua haki ya binadamu wote ni sawa…kuwafundisha vijana waweze
kuwa na uwelewa na kujitambua kuhusiana na masuala ya ardhi kuwawezesha wao
kuweza kuwaelekeza vijana wenzao lakini pia kwenda kutoa elimu kwenye jamii
kuweza kutatua migogoro iliyopo kwenye jamii”Alisema.