***************************
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Wananchi na wanachama wa CCM wametakiwa kutotengeneza Maadui na kuishi nao vizuri kwa ushirikiano ili kuwaonyesha CCM iliyo imara.
Kwa muktadha huo Tujihadhari na Maadui wa nje na ndani ambao wanataka kutufanya tugombane ili waweze kuuza silaha kwa kuwa wamoja na kujenga mashikamano ndani yetu.
Kauli hiyo imetolewa na Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga wakati akihutubia kwenye sherehe za miaka 43 ya chama cha Mapinduzi kwenye uwanja wa sheikh Amri Abeid Jijini Hapa na kuwataka wananchi kutunza siri za nchi zitakazo saidia kupambana na Maadui zetu.
Aliwaonya wanachama wa chama hicho kutofanya kampeni mapema na kusubiria muda utakapofika kwa chama hicho kinautaratibu wake iliojiwekea.
Alisema kuwa chama hicho kinajitegemea wala hakiombi fedha kutoka kwa wahisani kwa kuwa mapato yameongezeka kutoka bilion 30 hadi takribani bilion 900 na kina fedha za kushiriki uchaguzi bila kuomba msaada.
“Niwasihi wanachama wenzangu kuacha kufanya kampeni kabla ya wakati kwa kuwa chama chetu kina utaratibu wake” alisisitiza Kanali Ngemela.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mkoa huo Zeletho Stephen alisema kuwa chama hicho mkoa wa Arusha hakitarudia makosa ya mwaka 2015 na kuahidi ushindi kwenye uchaguzi wa mwaka huu siku ikifika.
Akawataka wanachama wa.chama hicho kujenga chama na kujitoa kwa nguvu kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi na kutuma salamu kwa mh.Raisi kuwa wanachama wa chama hicho hawatarudia kosa walilolifanya huko nyuma.