Baadhi ya wabunge wakipatiwa semina kuhusu kutumia kadi ya alama (score card) ili kupata takwimu sahihi ya mwenendo wa ugonjwa wa malaria iliyofanyika bungeni jijini Dodoma
Mbunge wa jimbo la Busega,Mkoani.Simiyu Mhe. Dkt. Raphael Chegeni,akizungumza kwenye semina kuhusu kutumia kadi ya alama (score card) ili kupata takwimu sahihi ya mwenendo wa ugonjwa wa malaria iliyofanyika bungeni jijini Dodoma
Mratibu wa Malaria na udhibiti wa wadudu wadhurifu Ofisi ya Rais, Tawala za Miko na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Bi. Stella Kajange,akizungumza mara baada ya kutoa semina kwa wabunge kuhusu utumiaji wa kadi ya alama (score card) ili kupata takwimu sahihi ya mwenendo wa ugonjwa wa malaria iliyofanyika bungeni jijini Dodoma
Sehemu ya waandaaji waa semina kwa wabunge yenye lengo la kuelimisha kuhusu kutumia kadi ya alama (score card) ili kupata takwimu sahihi ya mwenendo wa ugonjwa wa malaria iliyofanyika bungeni jijini Dodoma
Mwenyekiti wa wabunge wa chama cha kupambana na malaria (TAPAMA) Bi. Riziki Lulida ambaye pia ni Mbunge wa Lindi ,akizungumza kwenye semina iliyokuwa inawahamasisha wabunge kutumia kadi ya alama kupata takwimu sahihi juu ya kutokomeza ugonjwa wa malaria iliyofanyika bungeni jijini Dodoma
Mbunge wa jimbo la Busega,Mkoani.Simiyu Mhe. Dkt. Raphael Chegeni,akionyesha kadi ya alama (score card) jinsi ya kutumia ili kupata takwimu sahihi ya mwenendo wa ugonjwa wa malaria.
Mkurungezi wa Mkusanyiko wa Marais wa Afrika waliyoungana pamoja kutokomeza Malaria (ALMA) Bi. Joyce Kafanabo,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza kutoa semina kwa wabunge jinsi ya kutumia kadi ya alama (score card) ili kupata takwimu sahihi ya mwenendo wa ugonjwa wa malaria.
Wabunge pamoja na washiriki wa semina ya kutumia kadi ya alama (Score card) wakiwa katika picha ya pamoja bungeni jijini Dodoma
PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWEBLOG
……………………………………………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Wabunge wametakiwa kutumia kadi ya alama (score card) ili kupata takwimu sahihi ya mwenendo wa ugonjwa wa malaria katika kuandaa bajeti sahihi ili kuweza kutokomeza malaria nchini.
Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa wabunge wa chama cha kupambana na malaria (TAPAMA) Bi. Riziki Lulida ambaye pia ni Mbunge wa Lindi leo jijini Dodoma wakati wa kikao cha uhamashaji wabunge kutumia kadi ya alama kupata takwimu sahihi juu ya kutokomeza ugonjwa wa malaria.
Bi. Lulida amesema kuwa utumiaji wa kadi ya alama utasaidia wabunge na jamii kwa ujumla kupata takwimu sahihi juu ya malaria na kujua namna ya kuweza kujikinga na kujua mkoa gani unafanya vyema katika kutokomeza malaria.
Akizungumza Bi. Lulida amesema kwasasa mvua nyingi zinanyesha katika maeneo mengi hapa nchini hivyo kuna haja ya kusambaza vyandarua katika maeneo hayo kwani mvua hizo zinatengeneza mazalia ya mbu.
“Baadhi ya maeneo nchini yamepata mafuliko hivyo mamlaka husika wanatakiwa kugawa vyandarua katika maeneo hayo kwani mazalia ya mbu yatakuwa yameongezeka kutokana na mvua hizo”, ameeleza Bi. Lulida.
Naye Mkurungezi wa Mkusanyiko wa Marais wa Afrika waliyoungana pamoja kutokomeza Malaria (ALMA) Bi. Joyce Kafanabo amesema kuwa mfumo huo wa kutumia kadi ya alama unawasaidia wataalam wa malaria kuweza kujaza taarfa zao juu ya kutokomeza malaria na kujua mpango kazi gani ipo katika mfumo huo ili kutokomeza malaria.
“Wabunge ni wadau wakubwa kwani ni watunga sera na sharia za nchi hivyo wakipata kutumia kadi hii kwa ufasaha itasaidia katika kutengeneza bajeti zao katika kutekeleza majukumu yao katika kutokomeza malaria nchini” amesema Bi. Kafanabo.
Pia Bi. Kafanabo amesema kuwa wabunge wanawakilisha indadi kubwa ya watanzania hivyo watafanya uhamasijaji katika majimbo ili wapiga kura wao kuleta utekelezaji wa kutokomeza malaria kwa kutoa ushirikiano wakutosha kwa serikali na wataalamu kwa ujumla.
Kwa upande wake Mratibu Malaria na udhibiti wa wadudu wadhurifu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Bi. Stella Kajange ameeleza kuwa kadi ya alama itasaidia serikali kufatilia afua mbali mbali zinazotekelezwa na kufatilia utekelezaji wa kutokomeza malaria nchini.
“lengo ni kuhamasisha wabunge waweze kuielewa Malaria score card,na weweze kuitumia kufuatilia utekelezaji wa malaria katika mikoa na Halmashauri,pia lengo lingine ni kuhamasisha wabunge weweze kutetea bungeni bajeti yabutekelezaji wa afua za malaria iongezwe hasa kutokana na ongezeko la afua /intervention za malaria zilizoongezeka mfano upuliziaji wa viuadudu ktk mazalia ya mbu yaliyotambuliwa”amefafanua Bi Kajange.
Aidha Bi.Kajange amesema kuwa score card itawawezesha viongozi na watendaji katika ngazi ya kitaifa,Mkoa na Halmashauri kufanya ufuatiliaji wa karibu juu ya mwenendo wa utekelezaji wa afua(interventions)za malaria,kugundua changamoto,kuandaa mpango kazi na mikakati kwa ajili ya kutatua tatizo