Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akizungumza na Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya Habari katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere leo. Prof. Kabudi aliwaeleza Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya Habari kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika nchini mwezi Agosti 2019. Prof. Kabudi aliwasihi Wakuu hao kushirikiana na Serikali huusan katika kuelimisha umma kuhusu SADC pamoja na kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kuhusu fursa za mkutano huo na zile zinazopatikana katika nchi wanachama wa SADC.
|
Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Habari katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbas akitoa neno katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha Prof. Kabudi azungumze na Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya Habari nchini. Dkt. Abbas alimuhakikishia Mhe. Waziri kuwa namna anavyovijua vyombo vya habari vya hapa nchini vinavyofanya kazi hana shaka yoyote kuhusu kutoa ushirikiano wao. |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akisisitiza jambo kwa Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya Habari. |
|
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mhe. Paul Makonda akiongea na Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya Habari nchini. Mhe. Makonda alisema kuwa mkoa wa Dar Es Salam umejipanga kupokea ugeni mkubwa wa mkutano wa SADC ambao unakadiriwa utahudhuriwa na watu zaidi ya 1000 kutoka nchi 16 wanachama wa SADC. |
|
Meza Kuu kutoka kulia ni Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini, Bw. Henry Mwanika, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bi. Agnes Kayola, Waziri Prof. Kabudi, na Dkt. Abbas. |
|
Baadhi ya Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya Habari nchini walioshiriki katika kikao cha Waziri. Mwenye tai nyekundu ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania, Dkt. Ayoub Rioba. |
|
Mkutano wa Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya habari na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukiendelea |
|
Wakongwe wa tasnia ya Habari nchini ambao walikuwa walimu wa Mhe. Waziri katika fani hiyo. |
|
Picha ya Pamoja kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya Habari nchini. |