Baadhi ya marundo ya Taka katikati ya Jiji la Arusha kama yalivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha katika eneo la Kata ya Kaloleni jijini hapa picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.
…………………………………………………………………………………………………
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Halmshauri ya Jiji la Arusha inatuhumiwa kwa kushindwa kuzoa Taka katika jiji la Arusha kwa kipindi cha mwezi moja Sasa hali inayoonyesha kuhatarisha kupelekea kuzuka jwa magonjwa ya milipuko.
Kwa muda wa wiki takribani mbili chunguzi uliofanywa na mwanahabari hili kwenye kata mbalimbali za jiji la Arusha imekutana na msongamano wa marundo ya Taka kwenye Kata za Kaloleni Sinon Sokon 1 na Unga Ltd yakiwa yamezagaa baada ya magari kushindwa kuchukuwa taka hizo.
Hata hivyo Wafanyakazi wa usafi kwenye Kata za jiji hilo ikiwemo Kaloleni wamekuwa wakifanya usafi wakipangiwa maeneo makubwa hali inayowawia vigumu kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Akiongea mmoja wa Wafanyakazi hao aliekataa kutaja jina alisema kuwa utaona Mimi naanzia kufanya usafi kuanzia Stand Ndogo Hadi maeneo ya Polisi na kipato ni kile kile lote hilo ni eneo langu naiomba mamlaka kuangalia hilo.
Hata hivyo sehemu kubwa ya mitaro imejaa udongo hali inayopelekea maji kujaa barabarani hususani nyakati hizo za mvua zinazoendelea kunyesha kwenye maeneo mbalimbali mkoani hapa hali inayoonyesha maagizo ya waziri wa Tamisemi Suleiman Jaffo alitoyatoa kwa uongozi wa Jiji la Arusha kutotekelezwa kwa kipindi chote tokea mwaka Jana alipotembelea kuona ujenzi wa barabara ya dampo hadi Mrombo.
Kwa upande wake alipotakiwa kujibu suala hilo Afisa Mazingira wa Jiji la Arusha James Lobkok alijibu kwa ufupi kuwa atapiga baadae nae bibi Afya wa kata ya Kaloleni alipopigiwa simu ili kuweza kutoa majibu alisema kuwa atafutwe saa sita mchana atakuwa tayari kujibu suala hilo.