NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO
WAKAZI wa Vijiji na Vitongoji ,vinavyounda kata Jimbo la Bagamoyo Mkoani Pwani, watanufaika na usambazaji wa maji kutoka kwenye vyanzo vilivyopo kweye maeneo yao,kupitia mradi wa maji Chombe Juu.
Hayo yalibainishwa na Mbunge wa Jimbo hilo Dkt. Shukuru Kawambwa, akizungumza na wakazi wa Kitongoji cha Chombe Juu Kata ya Yombo, aliposhuhudia matofari na mabomba yatayojenga kituo cha kuchotea maji na mabomba ya kusambazia kwenye vituo vitatu.
Alisema , serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli, imedhamira kuwakomboa wananchi kwa kuwaondolea kero ya ukosefu wa maji safi na salama.
“Hapa nilileta wadau kuchimba visima viwili kwa thamani ya zaidi ya sh.milioni 9, lakini kwa bahati mbaya maeneo hayo moja halikuwa na maji ” alisema Dkt. Kawambwa.
Mhandisi wa maji (RUWASA)James Kionaumela aliishukuru serikali kwa kuanzisha chombo kinachoitwa RUWASA, kinacholenga kushughulikia usambazaji wa maji kutoka kwenye vyanzo na kuwasambazia wananchi.
Alielez, wamepewa jukumu la kuwasambazia maji wananchi, kutoka katika visima na kutandaza mabomba ili maji hayo yawafikie wananchi, na Chombe Juu wanapeleka matofali na mabomba kwa ajili ya kazi hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Bagamoyo, Mohammed Usinga alisema kuwa juhudi hizo zinalenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji.
“Tulikuja kutoka ahadi ya maji katika eneo hili, leo tumefika hapa chini ya Mkuu wetu wa msafara Dkt. Shukuru Kawambwa anayefanyakazi kubwa ya kuwatafuta marafiki kwa ajili ya kiiendeleza mradi wa maji uliopo kwnye eneo hill,” alisema Usinga.