Na. Joseph Mahumi, WF, Washington
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Timu ya Benki ya Dunia Tanzania, ikiongozwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Bw. Nathan Belete, kuhusu Ushirikiano wa Maendeleo kati ya Tanzania na Benki hiyo hususan Utekelezaji wa miradi inayotekelezwa nchini, pamoja na miradi inayotarajiwa kufadhiliwa na Benki hiyo kupitia mzunguko wa IDA 21, tukio lililofanyika kando ya Mikutano ya Kipupwe ya IMF na Benki ya Dunia, inayofanyika Jijini Washington D.C, nchini Marekani.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Fred Msemwa, Katibu wa Baraza la Mawaziri, Bw. Nsubili Joshua na Mshauri wa Mhe. Rais, masuala ya uchumi, Dkt. Blandina Kilama, na viongozi wengine waandamizi wa Serikali na Benki ya Dunia.











