Mabingwa wa Kihistoria timu ya Yanga imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kutoka Turiani Morogoro mchezo wa ligi Kuu Vodacom Tanzania bara uliomalizika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kipindi cha kwanza hakuna timu iliyoenda mapumziko ikiwa inaongozana kutokana na kushambuliana kwa zamu na kucheza mpira wa kuvutia kwa pande zote mbili.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko huku Yanga wakinufaika na mabadiliko hayo dakika ya 51 David Molinga aliwanyanyua mashabiki kwa kupachika bao nzuri akipokea pasi ya Ditram Nchimbi aliyetokea benchi.
Kwa ushindi huo Yanga imelipa kisasi cha kufungwa na Mtibwa Sugar kwenye Nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Mapinduzi Cup kwa njia ya mikwaju ya Penalti.
Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha Pointi 31 kwa kucheza mechi 16 nafasi ya nne huku Simba wanaongoza Ligi kwa pointi 47 mechi 18 na Azam Fc wakiwa nafasi ya pili pointi 37 kwa mechi 18 huku Namungo wakiwa nafsi ya tatu kwa Pointi 31 mechi 17 ,Yanga watashuka tena dimbani siku ya Jumatano kucheza na Lipuli Fc kutoka Iringa.
Matokeo ya mechi nyingine Azam Fc imeshindwa kutamba mbele ya Mbeya City kwa kulazimishwa sare ya 1-1,Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya KMC,Jkt Tanzania imeshindwa kutamba nyumbani kwa kufungwa bao 1-0 na ndugu zao Tanzania Polisi,