********************************
KAMPUNI ya bidhaa mbalimbali ya Unilever Tanzania
imezindua kampeni maalumu ya ya usafi miezi sita iitwayo ‘Omo Ng’arisha Festival’ itakayofanyika Tanzania nzima ikiwa na lengo la kuhamasisha faida, ubora na matumizi sahihi ya sabuni bora ya Omo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo katika Uwanja wa Mbagala Zakhem, Jiji la Dar es Salaam leo, Meneja Msoko wa bidhaa ya Omo, Bi. Upendo Mkusa alisema ni matumaini yao kwa kupitia kampeni hiyo jamii itatambua matumizi sahihi ili kupata matokeo yanayotarajiwa.
“Ni matumaini yetu watanzania watatumia sabuni ya Omo kwa usahihi kutokana na ukweli kuwa Omo Fast Action na Omo Extra Fresh ni bora katika kupambana na uchafu kwani ina nguvu zaidi ya mara 10 kuliko sabuni za kawaida na ni ukweli kuwa ukitumia Omo kufulia nguo za familia yako wewe na nguo za familia yako mtang’aa, nguo zako ziking’aa wewe na familia yako mtang’aa, tunataka kuona watanzania waking’aa,” alitanabaisha Bi. Upendo.
Akizungumza zaidi kuhusu kampeni hiyo, Bi Upendo alisema mara baada ya uzinduzi huo, kampeni hiyo itaendelea kwa matamasha na matukio mengine katika mikoa ya Dodoma, Dar, Mwanza, Arusha, Moshi na Mbeya.
Kuifanya kampeni hii kuwa yenye bashasha na mvuto,
Unilever imemtangaza Msanii maarufu nchini Tanzania, Bi. Isha Mashauzi kuwa Balozi wa Kampeni ya Omo Ng’arisha, atakayeshiriki katika matukio mbalimbali katika kampeni hii ikiwemo michezo, michezo ya kufurahisha na burudani ya muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali.
Kampeni itashirikisha timu ya promosheni ya Omo kwa kupita mlango kwa mlango majumbani, kwenye maeneo ya wazi na katika sehemu za biashara kuijulisha jamii juu ya ubora, faida na matumizi sahihi ya OMO, ambayo ni moja ya bidhaa kubwa zaidi ya Unilever.
Pamoja na hayo meneja huyo alisema kwa kutambua na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuendeleza uchumi wa viwanda na katika kuwaletea watu wake maendeleo, wameandaa zoezi maalumu la kuwatambua Wanawake Wajasiriamali 10 Bora
katika kila mkoa watakapofanya kampeni hiyo na kuwapa zawadi itakayowasaidia kuboresha biashara zao hivyo kuwafanya kung’aa.
“Ni imani yetu wanawake hawa miogoni mwao kuna wenye biashara ndogondogo, tutawatambua na kuwapa zawadi. Ni matarajio yetu utambuzi huu utaleta tija na kuwa kichocheo katika utendaji wao hivyo kukuza biashara zao.
“Unilever pia tupo mstari wa mbele katika kusaidia jamii, ni katika muskabali huo timu yetu ya kampeni katika mikoa hiyo niliyoitaja, tutatembelea katika mahospitali ambako tutaonyesha moyo wa kujali kwa kutoa msaada wa sabuni za Omo kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hizo tukiongozwa na balozi wetu wa Omo Bi. Isha Mashauzi.
“Unilever pia tunaunga mkono juhudi za serikali katika kuwataka wananchi kufanya usafi wa mazingira yao, na nina furaha kwamba kupitia kampeni ya Omo Ng’arisha katika kila mkoa timu yetu ya Omo Ng’arisha familia itashiriki katika shughuli za usafi kwa kushirikiana na viongozi wa mkoa huo,” aliongeza Bi. Upendo.
Aidha Meneja Masoko huyo alisema Unilever inatoa shukurani kubwa kwa ushirikiano inaoupata kutoka mamlaka mbalimbali za kibiashara na kiserikali hapa nchini.
“Tunaipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kuweka mazingira wezeshi na juhudi yake katika kuzifanyia kazi
changamoto mbalimbali zinazokabili jumuiya ya wafanyabiashara. Kwa upande wetu tunaahidi
kuongeza ubora wa bidhaa zetu kuhakikisha zinakidhi mahitaji ya wateja wetu, tukifanya biashara kwa kuzingatia kanuni na taratibu zote zilizopo huku tukiangalia namna bora zaidi ya kuinufaisha jamii ya watanzania,” alisema.
Licha ya bidhaa ya Omo ikiwa na aina mbili za Omo Fast Action na Omo Extra Fresh yenye nguvu mara kumi zaidi, Unilever inazo bidhaa nyingine kama; Sunlight-sabuni ya unga, inayotakatisha vizuri, yenye manukato na kulainisha ngozi, mafuta ya mgando na losheni ya Vaseline yenye
uwezo wa kutunza ngozi, Vim-sabuni ya kusafishia ambayo ni kiboko ya uchafu wa nyumbani, AXE-sprei ya mwili kwa wanaume inayokuacha na harufu nzuri kwa zaidi ya masaa 48 na Royco mchuzi mix, kiungo cha chakula chenye viungo asilia 16 kwa kuongeza ladha murua ya chakula.