Walimu wa shule binafsi nchini wamelalamikia kutokushirikishwa katika usimamizi wa mitihani ya kitaifa pamoja na usahihishaji licha ya kuwa nguzo muhimu katika maendeleo ya elimu nchini na kuchangia katika kukuza ubora wa elimu.
Akizungumza katika Mkutano wa Chama cha Walimu wa Shule binafsi nchini ,Katibu Mkuu wa Chama hicho Julius Mabula katika mkutano uliofanyika jijini Arusha ameiomba serikali iwashirikishe katika kusimamia na kusahihisha mitihani ya kitaifa kwani kwa miaka mingi wamekuwa hawashirikishi licha ya kuwa na sifa stahiki kama walimu wa shule za serikali.
“sisi tunasifa kama vile walimu wengine wa shule za serikali wanazo lakini kinachotushangaza atushirikishwi katika swala lolote la usahihishaji mitiani wala usimamizi wa hii mitiani kwa ufupi naweza sema tumetegwa sisi walimu wa shule binafsi “Julius Mabula
Amesema kuwa watafurahi sana kuona kwamba serikali inatambua uwepo wa kwa kuwashirikisha katika mambo mbalimbali ya uhusuyo elimu kwani nguzo muhimu katika maendeleo ya ellimu ni kushirikiana na kuchangia kukuza ubora wa elimu
Kwa upande wake mgeni rasmi,Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega amesema kuwa, serikali imepokea maombi ya walimu wa shule binafsi katika kusimamia mitihani ya kitaifa na watayafikisha kwenye ngazi husika ili yaweze kufanyiwa kazi
“tumesikia maombi yenu na tumeyapokea na napenda kuwahaidi kuwa tutafikiksha maombi haya katika ngazi husika ili yaweze kufanyiwa kazi hivyo niwaambie usiwe na hofu kwani serikali yenu ni sikivu na itafanyia kazi haya “amebainisha Kwitega.
Kwa upande wake Rais wa chama wa walimu wa shule binafsi nchini , Cornel Bukolo pamoja na wadau wa elimu wamesema kuwa, walimu wa shule binafsi wanapaswa kushirikishwa katika mipango ya kuboresha elimu na kupatiwa mafunzo ili kukuza kiwango cha elimu na kufikia nchi yenye uchumi wa kati .