Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema
Nchimbi akiwahutubia wataalam wa nchi nzima wa Idara ya Manunuzi wa
TANROADS walio katika mafunzo maalum ya mfumo rasmi wa kusimamia
mahitaji ya raslimali za matengenezo wa barabara (RMMS) kwenye ukumbi
wa VETA mjini Singida leo
Kaimu Meneja wa
TANROADS Mkoa wa Singida Injinia Matari Masige
(aliyesimama) akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi
(mwenye skafu) kuwahutubia wataalam
kutoka mikoa yote Tanzania Bara wa Idara
ya Manunuzi wa TANROADS walio katika mafunzo maalum ya ya mfumo rasmi wa kusimamia mahitaji
ya raslimali za matengenezo wa barabara (RMMS) kwenye ukumbi wa VETA
mjini Singida leo.Kushoto ni Mwezeshaji wa Mafunzo hayo Injinia Mussa George
Picha
ya pamoja baina ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi(mwenye
skafu) na wataalam wa nchi nzima wa Idara ya Manunuzi wa TANROADS walio
katika mafunzo maalum ya mfumo rasmi wa kusimamia mahitaji ya
raslimali za matengenezo wa barabara (RMMS) kwenye ukumbi wa VETA mjini
Singida leo
Na John Mapepele
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesema ili kuleta mapinduzi
makubwa kwenye sekta ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na
kukamilisha barabara zote nchini katika kiwango cha lami katika muda
mfupi ni muhimu Wakala wa Barabara nchini TANROADS iwashirikishe Wakala
wa Barabara vijijini na Mijini (TARURA) kwenye mafunzo maalum ya
kuboresha utendaji wa kazi yanayoendelea nchi nzima hivi sasa na
kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya hapa kazi tu.
Dkt.
Nchimbi ametoa rai hiyo leo kwenye ukumbi wa VETA mjini Singida
alipohutubia wataalam wa nchi nzima wa Idara ya Manunuzi wa TANROADS
walio katika mafunzo maalum ya ya mfumo rasmi wa kusimamia mahitaji
ya raslimali za matengenezo wa barabara (RMMS).
Amesema
ameshangazwa kuona katika mafunzo hayo muhimu katika sekta ya uboreshaji
miundombinu ya barabara kwa mfumo wa kisasa TARURA hawajashirikishwa
wakati mafunzo hayo ni muhimu na yanaongeza tija ya kazi zao.
“Najua nyie mmenolewa vizuri na baba yenu, Rais wetu mpendwa Dkt. John
Pombe Magufuli wakati akihudumu katika Wizara yenu, hivyo hakukuwa na
sababu yoyote ya kuwaacha wenzenu katika mafunzo hayo ili kubadirishana
uzoefu” alisisitiza Dkt. Nchimbi.
Alisema wataalam wa TANROADS
wanauzoefu mkubwa ambao kama watabadirishana na kushirikiana na TARURA
wataleta mapinduzi makubwa katika sekta hiyo kwani mfumo huo wa RMMS
unatumia raslimali chache na kuleta tija kubwa.
Aidha
alisema wakati mwingine kutokana na uzoefu mdogo kumekuwa na changamoto
za utengenezaji wa barabara za vijijini kwa wahandisi kuchukua muda
mrefu kukamilisha barabara hizo kwa kisingizio cha raslimali fedha
ambapo kama wangefundishwa mfumu huu wangeweza kuboresha utendaji wao wa
kazi.
Akimkaribisha Mkuu wa Mkoa kuwahutubia wataalam hao,
Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Singida, Injinia Matari Masige alisema
mafunzo ya mfumo wa RMMS ni nyenzo muhimu kwa tasnia ya ujenzi wa
miundo mbinu ya barabara na yanafanyika katika wakati mwafaka.
Alisema
kwa mfumo huo wa RMMS hakuna barabara katika nchi ambayo haitafikiwa
ambapo pia alisema faida kuu ya mfumo huu unasaidia kutambua mahitaji
halisi ya kila barabara hapa nchini.
“Kwa
mfumo huu hatutakuwa tena na kitu kama vile hakuna fedha ya ujenzi wa
barabara fulani. Sasa tatizo hilo limekwisha” aliongeza Injinia Masige
Mwezeshaji
wa mafunzo hayo Injinia Ndaji Mayige alifafanua kwamba kwa mfumo huo
kila sehemu korofi zitapata matengenezo kwa wakati na kwamba mfumo huo
unarahisisha utoaji wa taarifa za kila eneo.
Alikiri kuwa
mafunzo hayo ni muhimu kwa wakala zote mbili na kwamba wataangalia
namna bora ya kushirikisha TARURA ili waweze pia kupata mafunzo hayo
kwani yatasaidia kuboresha utendaji hadi katika ngazi za vijiji.
Injinia
Mayige alisema mafunzo hayo ni ya siku saba ambapo mafunzo kama hayo
tayari yameshatolewa kwa kada za Wakuu wa Idara za Mipango na Fedha na
Utawala nchi nzima.
Alisema nia ya mafunzo hayo kutolewa nchi nzima ili mikoa yote nchini kuwa na mfumo mmoja utakaorahisisha utendaji.