Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani,akizungumza na wakandarasi wanaotekeleza mradi wa REA awamu ya tatu, watendaji wa REA pamoja na Shirika la Usambazaji Umeme Tanzania (TANESCO),wenye lengo la kujadili utekelezaji wa usambazaji umeme vijijini mkutano huo umefanyika jijini Dodoma leo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga,akizungumza wakati wa kikao cha kujadili utekelezaji wa usambazaji umeme vijijini jijini Dodoma leo.
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani,alipokuwa akizungumza na wakandarasi wanaotekeleza mradi wa REA awamu ya tatu, watendaji wa REA pamoja na Shirika la Usambazaji Umeme Tanzania (TANESCO),kwa ajili ya kujadili utekelezaji wa usambazaji umeme vijijini kikao hicho kimefanyika jijini Dodoma leo.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja,akizungumza na wakandarasi wanaotekeleza mradi wa REA awamu ya tatu, watendaji wa REA pamoja na Shirika la Usambazaji Umeme Tanzania (TANESCO),wenye lengo la kujadili utekelezaji wa usambazaji umeme vijijini kikao hicho kimehudhuriwa na Waziri wa Nishati Dk.Kalemani jijini Dodoma leo.
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani,akisisitiza jambo alipokutana na wakandarasi wanaotekeleza mradi wa REA awamu ya tatu, watendaji wa REA pamoja na Shirika la Usambazaji Umeme Tanzania (TANESCO),wenye lengo la kujadili utekelezaji wa usambazaji umeme vijijini mkutano huo umefanyika jijini Dodoma leo kushoto kwake ni Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe.Subira Mgalu
PICHA ALEX SONNA-FULLSHANGWE BLOG
……………………………………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali imewaagiza wakuu wa wilaya na mameneja wanaosimamia Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini (REA) kuwakamata wakandarasi watakaoshindwa kutekeleza mpango kazi wa usambazaji umeme vijijini awamu ya tatu, mzunguko wa kwanza.
Hayo ameyasema leo jijni Dodoma Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani,wakati alipokutana na wakandarasi wanaotekeleza mradi wa REA awamu ya tatu, watendaji wa REA pamoja na Shirika la Usambazaji Umeme Tanzania (TANESCO), kujadili utekelezaji wa usambazaji umeme vijijini.
Waziri Kalemani amesema kuwa kila mkandarasi anapaswa kuwasilisha mpango kazi kuonyesha majina ya vijiji watakavyoenda kuwasha umeme kila na uwasilishe kwa wakuu wa wilaya.
Aidha Mhe.Kalemani amepiga maarufuku wakandarasi kusimamisha nguo za umeme bila kuweka nyaya,transform na kuwasha umeme kuanzia Februari 15 mwaka huu hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa mkandarasi atakayesimamisha nguzo kwa zaidi ya wiki moja bila kuwasha umeme.
”Hivyo nawaomba wakuu wa wilaya na Mameneja wa TANESCO fatilieni kama kuna mkandarasi husika anatekeleza mpango kazi wake kama alivyouwasilisha na achukue hatua ya kuwakamata wakandarasi watakaoshindwa kutekeleza mpango kazi wao”amesema Mhe Kalemani.
Waziri amsema kuwa kuna baadhi ya maeneo ambayo wakandarasi wamesimamisha nguzo bila kuweka nyaya, transfoma na kuwasha umeme, hivyo aliagiza mameneja kusimamia wakandarasi wawashe umeme haraka.
Aidha amesema kuwa malalamiko ya wakazi wa maeneo ya visiwani kuuziwa umeme kwa gharama kubwa, ni marufuku kwa wananchi wa maeneo ya visiwani kuuziwa umeme uniti moja kwa sh. 2500.
Dk.Kalemani amesema kuwa bei halali wanayopaswa kuuziwa umeme wananchi wa maeneo hayo ni sh. 100 kwa kila uniti moja.
“Nilipofanya ziara Ukerewe na Mafia nimekuta malalamiko hayo na Sasa naelekeza wateja wote wadogo ambao matumizi yao ya umeme ni chini ya uniti 75 kwa mwezi, malipo yao ni sh. 100 kwa kila uniti moja,” amesema
Awali , Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amos Maganga, amesema kuwa kumekuwa na utekelezaji hafifu wa mradi wa REA awamu ya tatu, kuanzia Januari mwaka huu.
Amesema kuwa kuanzia Januari hadi sasa ni vijiji 54 pekee ndivyo vilivyounganishiwa umeme, hivyo mkutano huo utatumika kubaini sababu za baadhi ya wakandarasi kushindwa kutekeleza mradi kama ilivyopangwa.