Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali imesema jumla ya watoto 36,548 wamepatiwa huduma mbalimbali zikiwemo huduma za kisaiklojia ,huduma za afya,huduma za elimu pamoja msaada wa kisheria katika kipindi cha Januari hadi Disemba mwaja Jana wakiwemo wa kiume 17,894 na wa kike 18,654 walitambuliwa ,kati ya hao jumla ya watoto 1,178 [wa kiume 768 na wa kike 410] walipatiwa huduma mbalimbali zikiwemo afya ,kisaklojia,kijamii na kuunganishwa na familia zao na kupatiwa elimu ya ujasiriamali.
Hayo yamebainishwa leo Januari 28,2020 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii ,jinsia ,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati akijibu Swali la mbunge wa viti Maalum Sikudhani Yasini Chikambo aliyehoji ,kumekuwa na wimbi kubwa la watoto wanaoishi mtaani ,ambao wanaishi katika mazingira magumu ,je,serikali ina mpango gani wa kuwasaidia watoto hao.
Katika Majibu yake,Naibu wa Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto ,Dkt.Faustine Ndugulile amesema serikali inatekeleza Program ya kuwaunganisha watoto na Familia na kuwatafutia malezi mbadala wale wasio na familia katika mkoa wa Mwanza.
Aidha,Dokta Ndugulile amesema Program hiyo ilianza kutumika mwezi Nov.2019 na inatarajia kufika mikoa yote ambayo ina wimbi la watoto wanaoishi mitaani huku pia akiikumbusha jamii kuwa jukumu la malezi,ulinzi na matunzo ya watoto ni la familia na jamii kwa ujumla.
Katika hatua nyingine Dokta Ndugulile amesema mamlaka za serikali za mitaa zinapaswa kusimamia sheria ya motto Na.21 ya mwaka 2009 ili kuwajibika wazazi kutekeleza majukumu yao badala ya kuwatelekeza watoto na kuwaacha wakizurura mitaani.