Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokuwa akifunga semina ya Viongozi wa Dola katika Usimamizi na Udhibiti wa Rasilimali Madini iliyofanyika jijini Dodoma
Waziri wa Madini Dotto Biteko,akizungumza wakati wa kufunga semina ya Viongozi wa Dola katika Usimamizi na Udhibiti wa Rasilimali Madini iliyofanyika jijini Dodoma
Sehemu ya washiriki wa semina ya Viongozi wa Dola katika Usimamizi na Udhibiti wa Rasilimali Madini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (hayupo pichani) wakati wa kufunga semina hiyo iliyofanyika jijini Dodoma.
PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWEBLOG
………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameviagiza Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhakikisha wanakuwa na kauli nzuri kwa wawekezaji hasa pindi wanapowakamata kwa makosa mbalimbali, huku akiitaka kufanya kazi kwa kushirikiana katika kulinda lasilimali za nchi.
Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo leo jijini Dodoma, wakati akifunga semina maalumu ya vyombo vya Ulinzi na Usalama inayohusu usimamizi wa Rasirimali Madini iliofanyika jijini hapa, iliyokuwa na lengo la kuwapa uelewa wa pamoja katika kulinda rasilimali za madini.
Majaliwa amesema vyombo vya Ulinzi na Usalama vinapaswa kuwa mstari wa mbele katika kulinda wawekezaji na pindi wanapokuwa wamewakamata wawekezaji kuwa na kauli nzuri ambazo hazitaleta usumbufu au kutoelewana na wawekezaji hao.
“Mara nyingi mnapowakamata hawa wawekezaji kauli zenu zinakuwa Kali sana, muwe na kauli nzuri ili kulinda masirahi ya pande zote mbili maana hata sisi bado tunawahitaji Hawa wawekezaji, ni Wajibu wenu kuhakikisha wanazijua sheria” amesema Waziri Majaliwa.
Aidha amesema ni wajibu wao kuhakisha huduma za vyakula migodini kuanzia sasa hazitoki nje ili bidhaa zetu zitumike katika utoaji huduma kwa wafanyakazi wa migodini.
“Unakuta mchele wanaoutumia wafanyakazi wa migodini unatoka nje jambo ambalo halikubaliki kwa sababu mchele tunalima sisi wenyewe, nyama inaagizwa nje wakati na sisi tunayo, hivyo naagiza suala hilo likafanyiwe mabadiliko,”amesema.
Amesema hakuna haja ya kuacha watu watumie bidhaa za nje katika vyakula wakati usalama wa chakula upo kwa asilimia zote.
“Baada ya mkutano huu naamini kila kitu kitabadilika hivyo ni vema mkalisimamie hilo katika migodi mbalimbali, “amesema Majaliwa.
Kuhusu maslahi kwa wafanyakazi wa migodi Waziri Mkuu Majaliwa amesema suala zima la stahiki kwa wafanyakazi ambao tayari wamemaliza muda wao kazini ili amalize akiwa amepata haki zake za msingi.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Majaliwa alimpongeza Rais Dk John Magufuli kwa mabadiliko aliyoyafanya katika sekta ya Madini na kupelekea mapato kuongezeka kutoka 194 bilion hadi 370 huku sekta hiyo ikishika nafasi ya pili ikiongozwa na Wizara ya Ujenzi.
“Hii inastahili pongezi sana Serikali inaweka jitihada kuhakikisha sekta ya madini inakuwa kwa kiasi kikubwa na kuongeza kuwa lengo kila mmoja apate stahiki “,amesema.
Kwa upande wa Waziri wa Madini Dotto Biteko amesema lengo la kuwakutanisha vyombo vyote vya ulinzi na usalama ni kuwapa uelewa wa pamoja katika kulinda lasilimali za madini bila kuingiliana baina ya vyombo hivyo.
Pia amesema semina hiyo haita ishia hapo kwani baadaye mwezi wa pili wataandaa semina nyingine kwa kila Mkoa ikihusishwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama kwenye mikoa hiyo na hao waliohudhuria semina hiyo ndio watakao kuwa wakitoa mafunzo kwa wengine.
Pia Waziri Biteko ametumia mda huo kuwatangazia vita watu wanaouza Madini feki na kuwataka waache mara moja Kutokana na kwamba weshagundua.
“Tunaomba wanaofanya hivyo waache mara moja tunaanza msako wa kuwatafuta watu wa aina hiyo kwa sababu Jambo hilo halikubaliki kabisa, “amesema Biteko.