NYOTA wa mpira wa vipaku nchini Marekani, Kobe Bryant na binti yake Gianna ni miongoni mwa watu tisa waliofariki katika ajali ya helkopta iliyotokea mji wa Calabasas, California jana asubuhi.
Bryant amefariki akiwa na umri wa miaka 41, alikuwa anasafiri na ndege binafsi aina ya helkopta ambayo ilianguka na kuwaka moto.
Mkuu wa polisi wa LA anasema kuwa hakuna yeyote aliyenusurika ajali hiyo.
Ripoti za awali zilisema kuwa kulikuwa na watu watano ndani ya ndege.
Bryant, ambaye ni bingwa wa NBA mara tano alikuwa anatambuliwa duniani katika historia ya kuwa mmoja wa wachezaji bora wa vikapu.
Salamu za rambirambi kutoka kwa watu maarufu na wachezaji wenzake nyota huyo zimekuwa zikimiminika kuonyesha mshtuko wa kifo cha nyota huyo wa mpira wa vikapu.
Kobe Bryant na binti yake mwenye umri wa miaka 13, Gianna wote wamefariki katika ajali Calabasas, California Jumapili asubuhi PICHA ZAIDI SOMA HAPA
Viwanja vyote vya mpira wa vikapu nchini Marekani vilitenga muda wa kuwa kimya kwa heshima ya mchezaji huyo.
Bryant atakumbukwa katika tuzo za Grammy(gat the Grammy Awards ) ambazo zilikuwa zikitolewa katika uwanja wa Los Angeles Lakers, eneo ambalo alikuwa akichezea kipindi chote.
“Tumechanganyikiwa na tuna uzuni sana kwa sasa,” alisema mtangazaji wa Grammys Alicia Keys.
“Kwa sababu mapema leo katika mji wa Los Angeles, Marekani na duniani kwa ujumla tumepoteza shujaa.
Tumesikitishwa sana kwa kumpoteza Kobe Bryant, ndio maana leo tumesimama katika nyumba aliyoijenga.”
NBA ilitoa tamko linalosema kuwa ,imesikitishwa sana na ajali iliyosababisha kifo cha Kobe Bryant na binti yake, Gianna” mwenye umri wa miaka 13.
“Kwa misimu 20 , Kobe alituonyesha kile ambacho kinawezekana kwa mtu ambaye ana kipaji na nia ya ushindi,” alisema.
Ajali ilitokeaje?
Afisa wa polisi Alex Villanueva alisema kuwa helkopta inaonyesha uwa na watu tisa wakati inaanguka, na kuondoa idadi ya watu watano ambao walitajwa hapo awali na maofisa.
Katika taarifa iliyotolewa na mji wa Calabasas zilisema kuwa wamepokea taarifa hiyo kwa maskitiko makubwa sana.
“Ndege hiyo ilianguka nje kidogo ya mji wa Las Virgenes majira ya asubuhi wa saa za Marekani . Hakuna aliyenusurika, aliongeza.
Gavin Masak, alikuwa anaishi karibu na eneo tukio hilo lilipotokea, alikiambia kituo cha CBS News kuwa helkopta ilianguka.
“Haukuwa kama mlipuko lakini tulisikia kama bomu limelipuka kwa sauti kubwa. Lakini ilisikika kama sauti ya ndege au helkopta, ilisikika sauti kubwa sana, niliingaia ndani na kwenda kumtaarifu baba yangu na kumwambia kilichotokea. Hivyo nilivyotoka nikaona moshi mweusi ukitokea mlimani, ulikuwa mweusi au kama kijivu”, alisema.
Shahidi mwingine alisema kuwa alisikia injini ikiwa inashida hata kabla ndege haijafika chini.
Polisi wa LA wameonyesha picha za tukio la ajali hiyo zikionyesha gari la zima moto na moshi ukivuka kutoka milimani.
Bodi ya taifa ya usafiri imeitambua ndege iliyoanguka kuwa ni Sikorsky S-76B na imesema kuwa itatuma kikosi chake kuchunguza chanzo cha ajali hiyo.
Bryant alikuwa nani?
Bryant alicheza mpira wa kikapu kwa 20-katika viwanja vya Los Angeles Lakers. Aliacha kucheza mpira huo Aprili 2016.
Mafanikio yake ni pamoja na kuwa mchezaji bingwa wa NBA kwa mwaka 2008, mara mbili aliibuka kuwa bora zaidi ya wengine.
Vilevile alikuwa mfungaji bora wa NBA pamoja na bingwa mara mbili wa mashindano ya Olympiki.