Mwenyekiti wa jukwaa la wakinamama kwenye ushirika Tanzania,Pilli Marwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha.


Happy Lazaro,Arusha.
Arusha .Wanawake wameshauriwa kuwa mstari wa mbele katika kuchaguana katika nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia ngazi za wilaya,mkoa na hata kitaifa ili kuongeza idadi ya wanawake viongozi katika maeneo yetu na kupata wawakilishi wa wanawake wa Ushirika Kila Mkoa.
Hayo yamesema mkoani Arusha na Mwenyekiti wa jukwaa la wakinamama kwenye ushirika Tanzania ,Pilli Marwa wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha kuhusiana na shughuli wanazofanya.
Amesema kuwa, umefika wakati sasa wa wanawake kuhakikisha wanasaidiana na kuchaguana wenyewe kwa wenyewe katika nafasi mbalimbali ili kuweza kupata uwakilishi wa kutosha katika ngazi mbalimbali .
Pilli amesema kuwa,lengo kuu la jukwaa hilo la wakinamama ni kuhakikisha wanawake wanapata haki zao za kiuchumi katika kumiliki haki mbalimbali za uongozi na kuhakilisha ile nafasi ya mwanamke katika jamii .
Ameongeza kuwa,wamepata fursa ya kushiriki katika maonesho hayo na wanawake wenzao kwenye ushirika na kuweza kutoa elimu kwa wananchi wanaofika kuweza kujua shughuli zinazofanywa na jukwaa hilo .
“Tanzania tuna jukwaa kitaifa ila kwa sasa hivi tunataka kuhakikisha kunakuwa na wawakilishi katika kanda mbalimbali ,mkoa na hata wilaya lengo likiwa ni kuhakikisha wanawake wanapata wawakilishi wao na mahali pa kuweza kusemea changamoto zinazowakabili.”amesema Pilli.
“Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitupatia shs Billion tano Mtaji wa Kukuza Bank ya Ushirikika kwani ni Rais anayejali watu sana hususan kwenye sekta ya kilimo.”amesema .
Ameongeza kuwa, hivi sasa wameanza mchakato wa kuchangua viongozi wa kanda ambapo watazunguka nchi nzima kuhakikisha wanapata viongozi wa kanda watakaosimamia majukwaa hayo katika kanda mbalimbali ambapo kwa baadaye watachagua viongozi hadi ngazi za mkoa na wilaya .
“Sisi kama jukwaa tumekuwa tukishwishi wanawake katika kujitokeza ngazi zote katika kugombea nafasi mbalimbali na sio kugombea tu bali hata kuwashawishi wanawake kuchaguana kwa wiki katika nafasi mbalimbali. “amesema .