


“Kwa hizi siku saba tulizokuwa hapa tumeweza kuwafikia wananchi 1844 na tumepokea migogoro 677 na kati yake tumefanikiwa kutatua migogoro 136 kwa kuwapatanisha na kutatua changangamoto zilizokuwa zikiwakabili,” amesema Msambazi
“Migogoro mingi imewasilishwa na wanaume, inawezekana wanaume wana changamoto zaidi kuliko wanawake lakini pia inawezekana wamebeba changamoto hizo kama baba wa familia ndio maana tumeona wengi wamejitokeza kuziwasilisha,”amesema .
Amefafanua kuwa asilimia kubwa wamefanikiwa kuitatua kwa pande zote mbili kuweza kukaa na kukubaliana na lile lengo ambalo kama serikali walipanga kulifikia limefanikiwa kwa sehemu kubwa na mingine inaendelea, kwani kuna zilizopo mahakamani lakinj mingine wanashughulikia kiutawala na itaendelea kufuatiliwa na yote itahitimishwa kwa jinsi ilivyo wasilishwa.
Ameongeza kuwa, wamewapa elimu juu ya msaada wa kisheria lakini pia kutatua migogoro ambapo wamemetumia nafasi hiyo kuwaandikia makubaliano, kuwawasilisha mahakamani wale ambao migogoro yao ilikuwa ina uhutaji wa kwenda mahakamani kwasababu kampeni imewajumuisha wadau kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo mawakili wa kujitegemea.
Msambazi amesema kuwa, lengo la kampeni hiyo ni kuhakikisha wanawa elimisha wananchi katika ngazi za kijamii kuhusiana na masuala mbalimbali ya kisheria na namna gani wanaweza kuifikia haki na kutatua migogoro ambapo hadi kufikia february 25,2005 wameshatekeleza kampeni hiyo mikoa 22.
Nao.baadhi ya wananchi waliojitokeza katika kampeni hiyo na kutatua migogoro yao wamemshukuru Rais Samia kwa kuleta wataalamu.wa kutatua migogoro ya ardhi mkoani Arusha ambapo wameweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa na kuomba zoezi hilo like linaletwa mara kwa mara kwani wananchi wengi wanateseka na hawana pa kukimbilia .