Kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, leo Machi 7 mwaka huu Wanawake kutoka Shirika la Mawasiliano Tanzani (TTCL) wameungana na Wanawake wenzao kutoka Taasisi, Mashirika, Kampuni na Sekta binafsi kufanya ziara maalum katika Hifadhi ya Ngorongoro ili kujionea uzuri wa urithi wa asili wa Tanzania.
Ziara hii imewapa fursa ya kujifunza kuhusu uhifadhi wa mazingira na namna sekta ya teknolojia inavyoweza kusaidia katika kulinda maliasili za Taifa.
Wakiwa hifadhini, walishuhudia wanyamapori mbalimbali kama vile simba, tembo, na faru weusi, Nyati, Swala, Pundamili na ndege mbalimbali huku wakijifunza kuhusu jitihada za kuhifadhi viumbe hao adimu.
Wanawake wa TTCL wameonesha utayari wao katika kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuitangaa sekta hii muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Kimataifa, 2025 yatafanyika jijini Arusha ambapo Mgeni rasmi anatajiwa kuwa Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yakibebwa na kauli mbiu “Wanawake na Wasichana 2025, Tuimarushe Haki, Usawa na Uwezeshaji”