Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma, Rwekaza Sympho Mukandala (katikati) akifungua mafunzo ya Baraza la Chuo Arusha. Kushoto ni Prof. Razack Lokina,, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma na kulia ni Prof. Winester Anderson, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Mipango.
….
Baraza za Chuo Kikuu cha Dodoma, tarehe 03 Machi lilianza mafunzo ya siku tatu ya Uongozi na uendeshaji bora wa Taasisi, yanayofanyika mkoani Arusha katika ukumbi wa Kimataifa wa AICC, kwa usimamizi wa Taasisi ya Uongozi.
Akifungua mafunzo hayo Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma, Rwekaza Sympho Mukandala, amewataka wajumbe na Menejimenti kuwa makini katika mafunzo hayo ili yasaidie kuongeza ufanisi, utendaji kazi na kuleta tija kwa Baraza la Chuo, katika kuisimamia Menejimenti katika masuala yote yanayohusu maendeleo na ustawi wa Chuo.
Miongoni mwa mambo yanayofundishwa ni Utawala bora wa Taasisi na Ustadi wa Viongozi, Changamoto zinazoendelea katika Utawala Bora na uelewa wa Masuala ya Kifedha, Ununuzi na Ugavi, Usimamizi wa Kimkakati wa Rasilimali za Umma, Usimamizi wa Mashirika na Usimamizi wa Vihatarishi.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma, Rwekaza Sympho Mukandala (katikati) akifungua mafunzo ya Baraza la Chuo Arusha. Kushoto ni Prof. Razack Lokina,, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma na kulia ni Prof. Winester Anderson, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Mipango.
Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano Kusiluka, aichangia jambo wakati wa Mafunzo ya viongozi Arusha.
Dkt. Kassim Hussein, Mkufunzi kutoka Taasisi ya Uongozi, akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma, Rwekaza Sympho Mukandala, wakati akiwawasilisha mada ya uongozi. Kulia ni Bi. Rhoda Aroko, Mkurugenzi wa Huduma za Wanafunzi.
Dkt. Kassim, akitoa mafunzo kwa washiriki Arusha.
Prof. Razack Lokina, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi, naye akichangia jambo wakati wa mafunzo ya uongozi Arusha.
CPA. Augustino Mbogella, Mkufunzi wa Masuala ya Usimamizi wa Vihatarishi na Udhibiti, akifundisha Viongozi wa Baraza na Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dodoma, kwenye Mafunzo yanayoendelea Arusha.