Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Viwanda, Biashara na Mazingira, Suleiman Saddiq,akiongoza semina ya wabunge iliyotolewa na Tume ya Ushindani (FCC) kwa kamati ya bunge ya viwanda,Biashara na Mazingira Bungeni jijini Dodoma.
Sehemu ya wabunge wakifatilia semina iliyotolewa na Tume ya Ushindani (FCC) kwa kamati ya bunge ya viwanda,Biashara na Mazingira Bungeni jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bw.John Mduma (wa pili kushoto) akifatilia hoja za wabunge wa kamati ya bunge ya Viwanda,Biashara na Mazingira katika kikao cha kamati hiyo ambapo wabunge wamepatiwa semina ya kutambua majukumu ya FCC,Bungeni jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Viwanda, Biashara na Mazingira, Suleiman Saddiq akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushauri wa kamati hiyo kwa Tume ya Ushindani (FCC) Bungeni jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) Bw.John Mduma akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoa semina kwa wabunge wa kamati ya kudumu ya bunge ya Viwanda,Biashara na Mazingira jijini Dodoma.
……………
Na.Alex Sonna,Dodoma
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara na Mazingira imeipongeza Tume ya Ushindani(FCC)kutokana na utendaji kazi wake huku ikiitaka kuongeza uelewa kwa wananchi juu ya bidhaa bandia ili kuweza kufikia uchumi wa viwanda.
Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Viwanda, Biashara na Mazingira, Suleiman Saddiq,jijini Dodoma mara baada ya semina ya kuwajengea uwezo wabunge na kuwasilisha mafanikio ya Tume katika kipindi cha miaka minne.
”Tume hii inafanya kazi nzuri ila mnapaswa kuongeza mkazo zaidi katika kujenga uelewa kwa wananchi”amesema Mhe.Saddiq
Mhe.Saddiq amesema kuwa wakati nchi inakwenda kwenye uchumi wa kati kupitia viwanda na kuwepo kwa hamasa ya wananchi kuanzisha viwanda ni lazima kuwe na ushindani wa haki kwenye soko.
” Sisi kama kamati tunaunga mkono juhudi hizi na tunawapongeza sana kwa kazi wanayofanya.lakini pia Kuna kila sababu ya Tume kuongeza kasi ya kutoa elimu kwa wananchi kuwa na elimu ya kutambua bidhaa bandia”amesisitiza
Awali Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bw.John Mduma,ameeleza mafanikio waliyoyapata katika kipindi cha miaka minne katika kudhibiti na kupambana na bidhaa bandia kwa kiasi kikubwa.
“Katika kipindi cha miaka minne tulishawahi kufanya elimu ya pamoja kati ya sisi na Shirika la Viwango Tanzania(TBS)na tulizunguka mikoa yote Tanzania Bara kutoa elimu kwa wazalishaji na walaji juu ya umuhimu wa kukataa bidhaa ambazo ni substandard ambazo ni bandia”amesema Bw.Mduma
Aidha amesema kuwa sasa kinankikosi kazi cha kitaifa kinachoundwa na wajumbe kutoka taasisi mbalimbali za TBS, TMDF, Polisi, ofisi ya mwanasheria wa serikali na ambao wamekua wakifanya ukaguzi wa mara kwa mara kupambana na bidhaa bandia.
FCC imepewa jukumu la kusimamia sheria mbili ,moja ni sheria ya ushindani inayoipa tume majukumu makubwa mawili ikiwemo kulinda ushindani sokoni na kumlinda mlaji na sheria ya pili ni sheria ya alama za bidhaa inayoipa tume nguvu ya kupambana na bidhaa bandia.