Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi,Mhandisi Isaack Kamwelwe akitoa hotuba wakati wa hafla ya utiaji saini ya mikataba mitano na kampuni za simu nchini kwa ajili ya kupeleka mawasiliano kwenye kata 252 nchini jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Dk.Joseph Kilongola akizungumza katika hafla ya utiaji saini ya mikataba mitano na kampuni za simu nchini kwa ajili ya kupeleka mawasiliano kwenye kata 252 nchini jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye,akizungumza katika hafla ya utiaji saini ya mikataba mitano na kampuni za simu nchini kwa ajili ya kupeleka mawasiliano kwenye kata 252 nchini jijini Dodoma.
Sehemu ya waalikwa waliohudhuria hafla ya utiaji saini ya mikataba mitano na kampuni za simu nchini kwa ajili ya kupeleka mawasiliano kwenye kata 252 nchini iliyofanyika jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu UCSAF Bi.Justina Mashiba,akizungumza katika hafla ya utiaji saini ya mikataba mitano na kampuni za simu nchini kwa ajili ya kupeleka mawasiliano kwenye kata 252 nchini jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Mawasiliano Bi.Maria Sasabo,akizungumza katika hafla ya utiaji saini ya mikataba mitano na kampuni za simu nchini kwa ajili ya kupeleka mawasiliano kwenye kata 252 nchini jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Miundombinu, Seleman Kakoso,akizungumza katika hafla ya utiaji saini ya mikataba mitano na kampuni za simu nchini kwa ajili ya kupeleka mawasiliano kwenye kata 252 nchini jijini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi,Mhandisi Isaack Kamwelwe,akiwa na viongozi waliosimama wakishuhudia utiaji saini ya mikataba mitano na kampuni za simu nchini kwa ajili ya kupeleka mawasiliano kwenye kata 252 nchini uliofanyika jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu UCSAF Bi.Justina Mashiba (kulia) akibadilishana mkataba na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Bw.Waziri Kindamba.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi,Mhandisi Isaack Kamwelwe akiwa katika picha ya pamoja na wabunge wa kamati ya kudumu ya Miundombinu wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe.Miraji Mtaturu wa pili kutoka kulia mara baada ya kushuhudia hafla ya utiaji saini ya mikataba mitano na kampuni za simu nchini kwa ajili ya kupeleka mawasiliano kwenye kata 252 nchini iliyofanyika jijini Dodoma.
…………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Ujenzi uchukuzi na Mawasiliano,Mhandisi Issack Kamwelwe, ameagiza mfuko wa Mawasiliano kwa wote, kuunda Kamati Maalamu ya kwenda kuchunguza minara yote ya makampuni ya Mawasiliano ili kubaini minara ambayo haifanyi kazi.
Waziri Kamwelwe, ametoa agizo hilo leo Januari 24, 2020, Jijini Dodoma wakati wa hafla ya kutuliana saini ya makubaliano baina ya Makampuni ya simu na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote, mkataba wa kupeleka mawasiliano Vijijini ambapo kata 252 hapa nchini zitafikiwa na huduma za Mawasiliano.
Waziri Kamwelwe amesema Kuna baadhi ya minara unatumia Nishati ya Solar na inafanya kazi mchana tu na pia ipo mingine haifanyi kazi kabisa na wananchi kukosa mawasiliano na kuagiza Mfuko wa Mawasiliano kwa wote kuunda kamati kuchunguza minara yote ambayo haifanyi.
” Yapo maeneo minara hiyo inaendeshwa kwa umeme wa Solar na kupelekea kufanya kazi mchana tu, na eneo lingine lipo Gairo hapo mnapopita kwenda Dar piteni mkaangalie, Leo naagiza muunde Kamati Maalamu kuchunguza minara yote ambayo haifanyi kazi kwa sababu hii mingine serikali imewekeza” amesema Kamwelwe.
Pia ameyataka Makampuni ya simu yaliyoshinda tenda ya kwenda kuweka minara hiyo kuhakikisha fedha zile zinalipwa kwenye serikali ya Kijiji na sio kwa mtu binafsi, ili serikali ikipata iwasaidie wananchi ambao mnafanya nao biashara.
” Kuna mazoea wataalamu wenu wanapokwenda sehemu hizo na kuona zinafaa wengi wananunua ardhi hiyo na wao ndio wanalipwa na kuacha wazawa wa pale hawanufaiki kwa lolote, tuna wabunge humu wengi wanalalamika mwaka mzima hawajalipwa sehemu hiyo ya fedha kumbe Kuna wachache wanaonufaika” amesema.
“Kuanzia leo ni marufuku na fedha hizo zilipwe kwenye serikali za vijiji ili nao ziwanufaishe, maana unakuta mmakonde ananufaika Katavi wakati wenyeji wa pale hawanufaiki kwa lolote, Mikataba yote isainiwe na kijiji”.amesema.
Pia amesema Kuna makampuni yanafanya mauziano na makubaliano ya mwanzo hawamwambii na akisha uziwa minara hawa wa Kijiji yule anakuwa hayatambui, na minara yote itakayojengwa kwa fedha za mfuko ni marufuku kubadilishana au kumuuzia bila ya kuwa serikali kujua.
Amesema yuko tayari kukaa na makampuni yote kujua changamoto zilizopo kwanini makampuni hayo yanafikia uamuzi wa kukabizi kwa makampuni mengine kusimamia minara hiyo kwa sababu wao wanafanya kazi na wananchi lakini kwenye makubaliano hayo wao hawanufaiki kabisa.
Aidha ameshukuru kwa kualikwa kushuhudia kutiliana mikataba hiyo ambayo itasaidia kata 252 zitanufaika ambapo kufikia octoba mwaka huu angalau wafikie asilimia 96 ya wananchi wawe na huduma za Mawasiliano.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote, Bi. Justina Mashiba, amesema wamesaini mikataba mitano 5 ambapo kata 252 na wananchi zaidi ya milioni tatu watanufaika na kupata Mawasiliano.
Ambapo amesema takribani kata 955 tayari zimeshapata dhabuni na Baada ya kukamilika wananchi wengi watafikiwa na huduma za mawasiliano, huku akibainisha lengo ni kuhakikisha kila mtanzania anafikiwa na Mawasiliano.
Makampuni yaliyoingia makubaliano na Serikali ni TTCL, VODACOM, AIRTEL, MIC, na VIATEL, ambapo TTCL imeshinda tenda ya kata 67, Airtel kata 9, Tigo kata 8, Viettel kata 114, na Vodacom kata 44.