NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Wanafunzi zaidi ya elfu 2423 wa shule za msingi na sekondari zilizopo Kata ya Tumbi katika Halmashauri ya Kibaha mji mkoani Pwani wamenufainika na kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Simia kwa kuweza kujengewa uwezo wa masuala mbali mbali yanayohusiana na haki zao za msingi ikiwemo suala zima la unyanyasaji wa kijinsia, kuepukana na kufanya vitendo vya mapenzi wakiwa shuleni ili kuepukaana kabisa na wimbi la mimba za utotoni.
Akizungumza na baadhi ya wanafunzi kuhusiana na kampeni hiyo Wakili George Banoba kutoka Wizara ya Katiba na sheria amesema kwamba wamefanikiwa kupita katika shule mbali mbali zikiwemo shule za msingi tatu pamoja na shule ya sekondari Mwanalugali kwa lengo la kuweza kutoa elimu ya masuala mbali mbali yanayohusiana na sheria.
Banoba amebainisha kwamba katika kampeni hiyo wameweza kuambatana na wadau mbali mbali wa sheria akiwemo pamoja na Afisa ustawi wa jamii pamoja na mkuu wa Dawati lajinsia Wilaya ya Kibaha kwa lengo la kuweza kupata elimu kwa wanafunzi na kuwaajengea uwezo juu ya kutambua haki zao za msingi ikiwemo mambo ya unyanyasaji wa kijinsia.
“Tumeanza rasmi kampeni yetu ya msaada wa kisheria ambapo tumeanza katika kata ya Tumbi na tumefanikiwa kuwafikia wanafunzi zaidi ya 2400 na wameweza kufundishwa masuala mbali mbali ya msaada wa kisheria bure na kwamba katika Halmashauri ya mji Kibaha watakwenda katika kata zipatazo 10 ambapo watatoa msaada wa kisheria katika maeneo ya migogoro ya ardhi, ndoa, miradhi, pamoja na usaidizi mwingine unaohusina na mambo ya kisheria,”amesema
Kwa upande wake Kaimu mkuu wa shule ya sekondari Mwanalugali Jeriko Rogers na pamoja na mwanafunzi wa shule hiyo Mwasalobo Komalumo wamempongeza Rais wa wawamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuanzisha kampeni ambayo itaweza kuwa ni mkombozi mkubwa katika kuwasaidia katika suala zima la msaada wa kisheria.

Naye Mkuu wa wa dawati la Kjinsia na watoto Wilaya ya Kibaha pamoja na Afisa ustawi wa jamii katika Halmashauri ya Kibaha mji wamebainisha kwamba kampeni hiyo itakwenda kuwa mkombozi na msaada mkubwa katika kuwasaidia wanafunzi pamoja na wananchi wengine kuweza kupata haki zao za msingi.
Kampeni ya msaada wa kisheria wa Mama Samia inaendelea kufanyika katika Mkoa wa Pwani ambapo itapita katika Halmashauri zote tisa kwa lengo la kuweza kutoa elimu ya masuala mbali mbali ikiwemo mambo ya migogoro ya ardhi, ndoa, mirathi pamoja na mambo mengine ya msingi yanayohitaji msaada wa kisheria.