NA MWAMVUA MWINYI
NAIBU Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amemuagiza mkandarasi wa kampuni ya Namis corporate ltd ambae anatekeleza mradi wa kusambaza umeme pembezoni mwa mji (Peri Urban )kukamilisha mradi huo ifikapo mei mwaka huu.
Aidha ameelekeza shirika la Umeme (TANESCO ),kuendelea na wajibu wa kusimamia miradi iliyoidhinishwa katika bajeti inayoendelea na ile ya 2020-2021 ili kuwatoa gizani baadhi ya wananchi ambao bado hawajafikiwa na huduma ya umeme.
Akizungumza huko Kimbiji -Kigamboni pamoja na Kitonga ,wakati alipokwenda kukagua miradi ya umeme na kujionea kazi inavyoendelea ,Mgalu amesema mkandarasi alisaini mkataba lakini analalamikiwa eneo la Msongola kuwa anasuasua hivyo ni lazima ahakikishe anamaliza kwa kipindi kilichopangwa bila kisingizio.
Hata hivyo, alielezea, kazi ya kufikisha umeme maeneo mbalimbali Kigamboni kupitia mradi wa Peri Urban unaohusisha mitaa 36 na kaya 1,200 ni mradi mkubwa na kazi inaendelea.
Mgalu alieleza ,kazi ya kufikishia umeme wananchi ni endelevu na serikali inatarajia kuanza rasmi kusambaza umeme kwenye vitongoji vyote nchini mara baada ya kumaliza kuufikisha katika vijiji vyote ifikapo Juni 2021.
Alisema ,serikali imewekeza katika nishati tilioni mbili mwaka wa fedha unaoendelea na ndio wizara iliyobeba bajeti kubwa ambapo kati ya fedha hizo bilioni 396 ni kwa ajili ya usambazaji wa umeme na sh.bilioni 86 mradi wa Peri Urban ambao ni mradi wa majaribio .
Mgalu alisema ,serikali imewekeza katika nishati tilioni mbili mwaka wa fedha unaoendelea na ndio wizara iliyobeba bajeti kubwa ambapo kati ya fedha hizo bilioni 396 ni kwa ajili ya usambazaji wa umeme na sh.bilioni 86 mradi wa Peri Urban ambao ni mradi wa majaribio katika maeneo ya Kigamboni,Ukonga,Kisarawe,Bagamoyo,Kibaha na Mkuranga.
Awali mkuu wa wilaya ya Kigamboni ,Sara Msafiri alishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kupatia umeme mitaa 36 kupitia mradi wa Peri Urban.
Sara alibainisha,pia wanashukuru bilioni 26 zilizoelekezwa katika ujenzi wa kituo kikubwa cha umeme Kigamboni ambapo yameshakamilika kwa asilimia 100.
Mwakilishi wa kampuni hiyo ya ukandarasi ,Yasin Hamad alisema amepokea maelekezo na watahakikisha wanamaliza kazi hiyo kwa wakati.