Mganga Mkuu Mkoa wa Iringa Dkt. Feith Mamkwe.
Mganga Mkuu Mkoa wa Iringa Dkt. Feith Mamkwe ametoa wito kwa Watoa Huduma za Afya kutoka Vituo vya kutolea Huduma za Afya kufanya Kazi Karibu na Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii(CHWs) katika utoaji wa Huduma za Chanjo .
Dkt. Mamkwe amebainisha hayo Mkoani Iringa katika Ufunguzi wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Watoa Huduma za Afya juu ya Uboreshaji wa Mawasiliano kati ya Mtoa Huduma na Mteja(Interpersonal Communication -IPC)katika Manispaa ya Iringa .
“Kati ya watu wanatusaidia sana kwenye masuala ya Huduma Mkoba na mambo mengine lukuki ya Afya ni Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii(CHW,s hivyo niwaombe kufanya nao Kazi kwa ukaribu sana wanapotoa Huduma nyumba kwa nyumba na Mitaa kwa Mitaa”amesema.
Aidha, Dkt. Mamkwe amewataka Wanufaika wa Mafunzo hayo wakiwemo Waganga Wafawidhi wa Vituo vya kutolea Huduma za Afya pamoja na Watoaji wa Huduma za Chanjo (Wachanjaji) kutumia Mafunzo hayo ya IPC ili kuboresha Huduma katika kuhakikisha kila mtoto anafikiwa na huduma za chanjo.
Kwa pande wake Afisa Programu kutoka Mpango wa Taifa wa Chanjo, Wizara ya Afya Enock Mhehe amesema Mafunzo hayo yana lengo la kupanua wigo katika Uboreshaji wa Huduma za Chanjo.
“Mafunzo haya yana lengo la kupanua wigo Utoaji wa Huduma za Chanjo hivyo, wakipata Mafunzo yataimarisha Mawasiliano baina ya Mtoa Huduma na Mteja”amesema Mhehe.