Ni kwamba Februari 16, 2025 saa 04:30 usiku huko Kitongoji cha Msia, Kata ya Chitete, Tarafa ya Bulambya Wilaya ya Ileje, Mkoa wa Songwe, Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kupitia taarifa za kiintelijensia pamoja na misako na doria za mara kwa mara zinazoendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na kushirikiana na Idara mbalimbali ikwemo Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA Wilaya ya Ileje limefanikiwa kumkamata Chisamba Siame Kameme (60) Mkukima, raia wa Nchi ya Malawi akiwa na vipande 18 vya meno ya tembo yenye thamani ya 84.2Kg na baada ya kufanya tathimini na wataalam ilionesha kuwa thamani ya meno hayo ni kiasi cha Shilingi Milioni 153,540,000 (Milioni Miamoja Hamsini na Tatu Laki Tano na Arobaini Elfu) ikiwa ni sawa na Tembo wa 03 na kila tembo 01 akiwa na thamani ya 51,180,000 (Milioni Hamsini na Moja Laki Moja na Themanini Elfu) alivyokuwa ameviweka kwenye mfuko wa salfet kisha kufunga kwenye baiskeli rangi nyeusi kwa lengo la kuviuza.
Aidha, Shauri la kesi hii upelelezi bado unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.