Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fatma Hamad Rajab, amesema Serikali inafanya juhudi mbali mbali kuhakikisha vijana wanapata nyenzo za kujiari wenyewe kupitia mafunzo ya amali.
Akizungumza na ugeni kutoka chuo cha Veta uliokuja Zanzibar kwa lengo la kubadilishana uzoefu kwa vijana kwenda kujifunza mafunzo ya amali, amesema hatua hiyo itasaidia kuwa na wataalamu katika sekta mbali mbali pamoja na kuongezeka kwa fursa za ajira.
Aidha amesema Serikali inachukuwa juhudi mbalimbali kuhakikisha Vijana wanapata nyenzo kujiajiri wenyewe kupitia mafunzo ya amalina kupata ajira ili waweze kuachana na Vitendo Viovu ikiwemo utumiaji wa Dawa za kulevya,Bangi na Dawa za kulevya.
Ujumbe huo pia umefanya ziara katika maeneo mbali mbali ikiwemo kituo cha mafunzo ya vijana Bweleo , uwanja wa Amani Complex na kumalizia katika viwanja vya michezo Maisara pamoja na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu CCM, Nd. Mohammed Said Dimwa .