Na Prisca Libaga Arusha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 03.02.2025 imeshiriki Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Sheria wilayani Longido katika Jengo la Mahakama ya Wilaya ya Longido.
Kauli Mbiu ya Maadhimisho hayo kwa mwaka 2025 ilikuwa ni; *_”Tanzania ya 2050; Nafasi ya Taasisi Zinazosimamia Haki Madai Katika Kufikia Malengo Makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo”_*
Mgeni rasmi alikuwa ni Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Longido Mhe. Eliarusia Nassary na mgeni maalum alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Salum Kali. Aidha, washiriki wa maadhimisho hayo zaidi ya 50 walipewa elimu juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya na kuelezewa ukali wa Sheria kuwa ukikamatwa unajihusisha na dawa hizo unaweza kufungwa miaka 30 au maisha jela.
Ofisi ya Mamlaka Kanda ya Kaskazini iliwahamasisha wananchi kuendelea kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa hizo kupitia namba ya simu ya bure ya 119*