Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho katikati,akiongoza matembezi ya Wanachama wa Chama hicho wa Wilaya ya Tunduru Namtumbo yaliyofanyika kwa lengo la kuunga mkono azimio la kumpitisha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea Urais wa Tanzania na Dkt Hussen Ali Mwinyi kuwa Mgombea Urais wa Zanzibar,kulia kwake Mjumbe wa Halmashauri kuu Hemed Challe.
Mjumbe wa Halmashauru Kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma Hemed Challe,akisalimiana na Wanachama wa CCM wa Wilaya ya Tunduru kabla ya kufanyika matembezi ya kuunga mkono azimio la Chama hicho kumpitisha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea Urais wa Tanzania na Dkt Hussen Mwinyi kugombea Urais wa Zanzibar.
Wananchma wa Chama cha Mapinduzi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho(hayupo pichani)wakati akihutumia Mkutano maalum wa kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea Urais wa Tanzania na Dkt Hussen Mwinyi kugombea Urais wa Zanzibar,mkutano uliofanyika katika Uwanja wa CCM Tunduru mjini.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho,akipokea Picha ya Rais wa Zanzibar Dkt Hussen Mwinyi kutoka kwa Mwanachama wa Chama hicho Happy Mpakate, kwenye mkutano maalum wa kuunga mkono azimio la kumpitisha Rais Samia Suluhu Hassan kugombea Urais wa Tanzania na Dkt Hussen Mwinyi kugombea Urais wa Zanzibar katika Uchaguzi wa Mwezi Oktoba Mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma Simon Chacha,akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita iliyotekelezwa katika Wilaya hiyo kwenye Mkutano maalum wa kuunga mkono azimio la kumpitisha Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea Urais wa Tanzania na Dkt Hussen Mwinyi kuwa Mgombea wa Urais wa Zanzibar katika Uchaguzi utakaofanyika baadaye mwaka huu.
Na Mwandishi Wetu,
Tunduru
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho alisema,maamuzi ya kuwapitisha Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea Urais wa Tanzania na Dkt Hussen Mwinyi kupeperusha Bendera ya Chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu ni sahihi kutokana na mambo makubwa waliyoyafanya kwa Watanzania.
Mwisho,amewataka Wakazi wa Mkoa wa Ruvuma kutembea kifua mbele kutokana na maendeleo makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Aidha,amewasisitiza Wakazi wa Mkoa huo kutumia muda wao kujikita kwenye shughuli za uzalishaji mali hasa kilimo kwani Serikali imewekeza nguvu kubwa kwa kutoa pembejeo za ruzuku bure kwa Wakulima ili kuongeza uzalishaji na kuleta tija kwa Wakulima.
Katika hatua nyingne Mwisho,amewaagiza maafisa kilimo na maafisa Ushirika Mkoani Ruvuma, kuhakikisha wanatenda haki kwenye suala la ugawaji wa pembejeo kwa kuhakikisha kila mkulima ananufaika na matunda ya Serikali yake badala ya kugawa pembejeo hizo kwa upendeleo.
Pia,amewakumbusha Wanachama wa Chama hicho kutimiza wajibu wao kwa kueleza mambo mazuri yaliyofanywa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ili Wananchi wafahamu maendeleo yaliyofanywa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi katika kipindi cha miaka minne badala ya kukaa kimya.
Amewashukuru Wananchi wa Wilaya ya Tunduru kwa maamuzi sahihi kwa kuwachagua wagombea wa CCM kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika mwaka uliopita ambapo Chama hicho kilipata ushindi ushindi wa kishindo.
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Simon Chacha alisema,katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wamepokea zaidi ya Sh.bilioni 300 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kwa mujibu wa Chacha,fedha hizo zimetumika kutekeleza miradi maji,elimu,afya,umeme,Barabara,Mawasiliano,Utumishi na Utawala Bora na kuwezesha Wananchi wa Wilaya ya Tunduru kupata huduma bora za kijamii,kisiasa na Kiutamaduni.
Alisema,Sh.bilioni 5,598,853,033.85 zimetumika kujenga miundombinu ya vyumba vya madarasa,maabara za sayansi,mabweni,miundombinu ya vyoo na maji kwenye shule za Sekondari na Sh.bilioni 2,545,934,950.50 zimetumika kujenga miundombinu kama hiyo katika shule za msingi.
Katika sekta ya afya alisema,wamepokea Sh.bilioni 3,155,923,169.67 kujenga zahanati,vituo vya afya,nyumba za Watumishi,miundombinu ya vyoo na maji na Sh.bilioni 1,106,017,026.21 zimetumika kwenye mpango wa uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia mapato ya ndani(mikopo ya asilimia kumi).
Aidha,Halmashauri ya Wilaya imetumia Sh.bilioni 11,346,151,952 kuwezesha mpango wa kunusuru kaya maskini(Tasaf) ,elimu bila malipo kwa shule za Sekondari,ujenzi wa miundombinu shule za msingi(BOOST)na pembejeo za kilimo.
Alisema,Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa) umepokea Sh.8,271,911,919.52,TARURA Sh.bilioni 10.500,Mamlaka ya maji Tunduru mjini Sh.bilioni 3.9,Tanesco Sh.bilioni 10.490,umeme vijijini(REA)Sh.bilioni 11.984 na miundombinu ya umeme Imara Sh.bilioni 245.980.
Naye Katibu Tawa la wa Wilaya ya Namtumbo Fransis Mgoloka alisema,katika kipindi cha miaka minne Wilaya hiyo imepokea zaidi ya Sh.bilioni 46.554 kati ya hizo Sh.bilioni 3.351 zimekwenda kwenye sekta ya afya,elimu Sh.bilioni 9, Sh.bilioni 8 umeme vijijini(REA) na sekta ya maji Sh.bilioni 7.8.