Wabunge mmetenda uungwana mkubwa sana kwa mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusukuma mipango ya serikali kwaajili ya kuwahudumia wananchi lakini pia Bunge hili limethibitisha uungwana na ustarabu na leo tunakuunga mkono, tunakutia moyo, tunakuombea, tunakutakia mema na matashi yetu kwa Rais wetu ni kuona tanzania inaendelea” Mhe. Dkt. Doto Biteko.
Dkt.Biteko ameyasema hayo leo 31 Januari 2025 wakati akichagia azimio la bunge la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa Nishati Afrika (Mission 300) uliofanyika jijini Dar es Salaam.