********************************
Na Silvia Mchuruza.
Bukoba.
Mkuu Wa Mkoa Kagera Brigedia General Marko Elisha Gaguti amewaapisha wajumbe wapya wawili wa baraza la aridhi na nyumba katika ukumbi wa ofisi za Mkoa katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.
Akizungumza na wajumbe wa sheria, viongozi wa dini, pamoja na maafisa usalama wa mkoa wa kagera Mkuu wa mkoa amewataka wajumbe wapya wa baraza la aridhi na nyumba kutenda haki katika utendaji wao wa kazi hili kuhakikisha wanaleta amani katika jamii na siyo migogoro.
“Leo mmepata dhamana kubwa katika kusimamia nakutatua migogoro ya aridhi mkahakikishe mnafanya kazi na kutoa ushirikiano mzuri kwa wananchi ili muweze kuleta amani pasipo na amani” alisema Rc Gaguti.
Nae jaji mfawidhi mahakama kuu kanda ya bukoba Bi.Luccia Kalio amewataka wajumbe wapya walioapishwa Leo kuhakikisha wanatenda haki huku akisema kuwa mkoa wa kagera unaongoza kwa asilimia 40% na zaidi unakumbwa na migogoro ya aridhi na nyumba ikiwa wilaya ya kwanza ni missenyi ikifuatiwa na halmashauri ya Bukoba manispaa kutokana na watumishi baadhi kula rushwa.
Aidha sambamba na hayo amemtamburisha jaji mpya kutoka kanda ya bukoba Bi. Angle Anthony Bahati ambae ameteuliwa na Rais wa awamu ya tano mwezi November mwaka Jana ambapo nae Bi. Angle amewataka kwa ufupi wajumbe hao wapya kutoka ushirikiano mzuri ili hata ngazi za juu wafanye kazi kwa weledi zaidi.
“Mimi niwaombe tu wajumbe hawa walioapishwa leo kutoka ushirikiano mzuri hili hata sisi wa ngazi za juu tuweze kufanya kazi vizuri na pia nawashukuru wadau wrote maana Leo ndiyo mala yangu ya kwanza kusimama na kuongea na viongozi kama hivi kwahiyo nawashukuru sana”.alisema Bi. Angle.