Naibu Makamu Mkuu wa taaluma- utafiti na ushauri elekezi Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Razack Lokina akizungumza na wachina pamoja na wanafunzi wanaojifunza kichina kwenye maadhimisho ya mwaka mpya wa Kichina unaojulikana kama mwaka wa Nyoka.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
Vijana nchini wamehimizwa kuendelea kuenzi utamaduni za kitanzania popote wanapokuwa na kutokuusahau asili ya walipotoka kwani ndiyo sababu ambayo imewapelekea wengi wao kulalamikiwa kuporomoka kwa maadili yao.
Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma na Naibu Makamu Mkuu wa taaluma- utafiti na ushauri elekezi Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Razack Lokina kwenye maadhimisho ya mwaka mpya wa Kichina unaojulikana kama mwaka wa Nyoka ikiwa ni sehemu ya kudumisha utamaduni wao yaliyoandaliwa na taasisi ya conficius katika chuo hicho.
“Kwangu mimi au kwa chuo tunaona huu ni utaratibu mzurikwasababu unaomfanya mtu popote alipo duniani kuweza kudumisha utamaduni wake na hapa tumeona bila kusahau tunaona kizazi cha sasa hivi kina tabia ya kujisahau lakini tumeona wenzetu wa kichina muda wote wanaendelea kudumisha utamaduni wao tangu enzi na enzi,”amesema.
Aidha, Prof. Lokina ameipongeza Serikali kwa kurudisha somo la historia shuleni ambalo linawakumbusha wanafunzi walipotoka ili waweze kuendelea kuishi kwenye utamaduni wao licha ya kuwa kwasasa dunia ipo kwenye maendeleo ya sayansi na teknolojia lakini wasisahau mababu zao waliishi vipi ili kulinda maadili.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkazi wa taasisi ya lugha na utamaduni wa kichina UDOM Dkt. Rafiki Sebonde amesema mwaka mpya wa kichina ni tofauti na miaka mingine kwani wao usherehekea miaka yao mipya kwa kufuata aina za wanyama, hivyo mwaka huu kwao ni mwaka wa nyoka kwa njisi karenda yao ilivyo.
“Mwaka mpya wa Kichina tofauti na karenda za mataifa mengine ni kwamba wao wanaposherehekea ukusanyika kwa pamoja na kuwa suala la kifamilia zaidi na wanapokutana usherehekea kufanikia kwao kwa mwaka mwinginena uliopita na kula vyakulaa maalum wanavyopaswa kula kwahiyo hapa leo tunasherehekea mwaka huu mpya tukiwa tumeandaa chakula cha kichina pamoja na kufanya matukio mbalimbali,”amesema.
Ameongeza kuwa wanaposherehekea na Wachina wanajifunza kuwa mtu akiwa sehemu yoyote hapaswi kusahau maadali yake kwani yapo kwa namana mbalimbali ikiwemo kuvaa, kula, heshima na hata kuzungumza na watu wenginevile vitu ambavyo anakuwa amejifunza kutoka kwa wazazi hata akiwa mbali anapaswa kuendelea kuvitunza na kuvilinda kama wanavyofanya wengine.
Naibu Makamu Mkuu wa taaluma- utafiti na ushauri elekezi Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Razack Lokina akizungumza na wachina pamoja na wanafunzi wanaojifunza kichina kwenye maadhimisho ya mwaka mpya wa Kichina unaojulikana kama mwaka wa Nyoka.
Mkurugenzi mkazi wa taasisi ya lugha na utamaduni wa kichina UDOM Dkt. Rafiki Sebonde akizungumza na wachina na wanafunzi wanaosoma kichina kwenye maadhimisho ya mwaka mpya wa Kichina unaojulikana kama mwaka wa Nyoka.
Wanafunzi wanaosoma Lugha ya kichina wakicheza nyimbo za kichina kwenye maadhimisho ya mwaka mpya wa Kichina unaojulikana kama mwaka wa Nyoka.
Wachina na wanafunzi wanaosoma lugha ya kichina kwenye maadhimisho ya mwaka mpya wa Kichina unaojulikana kama mwaka wa Nyoka.