Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma wakati
akiwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kushiriki
Maadhimisho ya Miaka 25 ya Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania
(TAWJA) leo tarehe 20 Januari 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdallah wakati
akiwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kushiriki
Maadhimisho ya Miaka 25 ya Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania
(TAWJA) leo tarehe 20 Januari 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Jaji Mkuu wa
Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdallah, Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na
Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Barke
Sehel pamoja na viongozi mbalimbali katika Maadhimisho ya Miaka 25 ya Chama cha
Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) yaliyofanyika katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) leo tarehe 20 Januari 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
akihutubia wakati wa Maadhimisho ya Miaka 25 ya Chama cha Majaji na Mahakimu
Wanawake Tanzania (TAWJA) yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
cha Arusha (AICC) leo tarehe 20 Januari 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
akimkabidhi zawadi mmoja wa waanzilishi wa Chama cha Majaji na Mahakimu
Wanawake Tanzania (TAWJA) Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Eusebia Munuo
wakati wa Maadhimisho ya Miaka 25 ya Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake
Tanzania (TAWJA) yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha
(AICC) leo tarehe 20 Januari 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
akimkabidhi zawadi Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma
iliyotolewa na Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) wakati
wa Maadhimisho ya Miaka 25 ya Chama hicho yaliyofanyika katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) leo tarehe 20 Januari 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Jaji Mkuu wa
Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdallah, Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na
Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Barke
Sehel pamoja na viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja na Waanzilishi wa
Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) wakati wa
Maadhimisho ya Miaka 25 ya Chama hicho yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano
cha Kimataifa cha Arusha (AICC) leo tarehe 20 Januari 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Jaji Mkuu wa
Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdallah, Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na
Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Barke
Sehel pamoja na viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chama
cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) wakati wa Maadhimisho ya
Miaka 25 ya Chama hicho yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha
Arusha (AICC) leo tarehe 20 Januari 2025.
……….
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
ametoa wito kwa Watanzania wote kuibua taarifa zinazohusu vitendo vya ukatili ili
hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi ya wahusika.
Makamu wa Rais ametoa wito huo alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Miaka 25 ya
Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) yaliyofanyika katika
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) leo tarehe 20 Januari 2025.
Amesema wapo wanawake, watoto na wanaume wanaopitia vitendo vya ukatili wa
kijinsia au kimwili lakini hawatoi taarifa kwenye vyombo vya sheria, vilevile baadhi ya
mila na desturi zimekuwa zikitumika kuwakandamiza waathirika.
Amesema pamoja na dhamira njema ya Serikali ya kuhakikisha usawa wa kijinsia
hapa nchini, bado wanawake ambao idadi yao ni zaidi ya nusu ya watu hapa nchini,
wanapewa nafasi ndogo katika umiliki wa mali na wanabaguliwa kwa msingi wa
jinsia.
Ameongeza kwamba kwa mujibu wa Mpango wa Kitaifa wa Kupinga vitendo
vya Kikatili dhidi ya Wanawake wa mwaka 2016, kati ya wanawake kumi, 4
wamepitia ukatili wa kimwili, na mmoja kati ya watano wamepitia ukatili wa kingono
miongoni mwao wakiwa na umri mdogo (chini ya miaka 15).
Halikadhalika, Makamu wa Rais amesema kulingana na Ripoti ya UN Women Social
Institution and Gender Index (SIGI) 2022, ukatili wa kijinsia nchini Tanzania
unabainishwa zaidi kupitia ndoa za utotoni, ubaguzi ndani ya familia, ukatili dhidi ya
wanawake, ukosefu wa uhuru katika kupanga uzazi, upatikanaji na umiliki wa ardhi.
Pia kulingana na Taarifa ya Tathmini ya Ukatili wa Kijinsia Tanzania iliyoandaliwa na
Benki ya Dunia mwaka 2022, 40% ya wanawake wote wenye umri wa miaka 15 hadi
49 wamefanyiwa ukatili wa kimwili na 17% wamepitia ukatili wa kingono.
Aidha Makamu wa Rais amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
imejizatiti kuimarisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake hapa nchini
kwa kuanzisha Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambayo
inasimamia masuala ya usawa wa kijinsia.
Amesema dhamira hiyo ya Serikali
inaonekana zaidi kupitia mikakati, mipango na sera za kitaifa kama vile Dira ya
Maendeleo ya Taifa 2025, Mipango ya Maendeleo ya Taifa ya Miaka Mitano, Mkakati
wa Kitaifa wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini (NSGR) na Sera ya
Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya 2000.
Ameongeza kwamba, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt.
Samia Suluhu Hassan, imedhihirisha kwa vitendo dhamira yake ya kuboresha
utendaji katika utoaji haki, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha usawa wa kijinsia katika
ngazi mbalimbali za uongozi wa Mahakama ambapo kwa takwimu, Mahakama ya
Rufani, 33% ya Majaji ni wanawake, Mahakama Kuu, ni 38%.
Kwa Wasajili wa Mahakama ,wanawake ni 33% na Naibu wasajili ni 48.72%. Aidha, wanawake ni
50% ya Mahakimu wa Mahakama za Mahakimu Wakazi na 41% ya Mahakimu wa
Mahakama za mwanzo.
Makamu wa Rais ametoa wito wa kujenga tabia ya kutambua na kusheherekea
mafanikio ya wanawake katika jamii ili kutoa hamasa kwa wasichana na wanawake
wengine kujifunza na kuiga mifano hiyo.
Amesema ipo mifano ya wanawake hapa
nchini waliofanya vizuri katika fani mbalimbali kwa kuanza na Rais Mheshimiwa Dkt.
Samia Suluhu Hassan, Rais wa kwanza mwanamke; Bibi Titi Mohamed, mwanamke
aliyekuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru wa nchi pamoja na wengine
wengi.
Aidha amesisitiza umuhimu wa Majaji na Mahakimu wanawake nchini walioko katika
utumishi na waliostaafu, kuhakikisha wanajiunga au wanahuisha uanachama wao wa
TAWJA kwa kulipa ada. Amesema TAWJA inahitaji mshikamano na ushiriki wa
wanachama wake wote ili kufikia malengo yake.
Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma
ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa dhamira njema na kuendelea
kuiwezesha Mahakama ambapo Majaji wa Mahakama ya Rufani wameongezeka
kutoka Majaji 17 mwaka 2021 hadi Majaji 40 mwaka 2025.
Mhe. Prof Juma amesema ni jukumu la Majaji na Mahakimu kuitumia Dira ya
Maendeleo ya Taifa 2050 ili kufikia malengo yaliyotajwa ikiwemo vipengele vyote
vinavyotaja masuala ya kijinsia na kisheria.
Awali akitoa taarifa, Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake
Tanzania (TAWJA) Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Barke Sehel amesema
mafaniko yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 25 ya TAWJA yanatokana na
mifumo imara ya usawa kijinsia hapa nchini pamoja na ushirikiano mzuri kutoka
katika Serikali na Mahakama ya Jamhuri ya Tanzania na Mahakama ya Zanzibar.
Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) kilianzishwa mwaka
2000 ambapo kinasherehekea Jubilei ya miaka 25 yenye kauli mbiu isemayo “Jubilei
ya Miaka 25 ya TAWJA: Kusherehekea Utofauti na Mshikamano katika Usawa wa
Kijinsia”
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
20 Januari 2025
Arusha.