Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wataalamu wa afya kutoka Hospitali Fuwai iliyopo Beijing China leo wakati wataalamu hao walipofika JKCI kwaajili ya kubadilishana ujuzi na wenzao wa JKCI katika kutoa huduma za upasuaji mdogo wa moyo bila kutumia mashine ya mionzi kwa watoto wenye magonjwa ya moyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Fuwai iliyopo Beijing China prof. Xiangbin Pan akielezea namna huduma za upasuaji mdogo wa moyo bila kutumia mionzi zinavyoweza kufanyika kirahisi kutokana na maendeleo ya teknolojia wakati wa mafunzo ya jinsi ya kuziba matundu na kuzibua mishipa ya damu ya moyo iliyoziba bila kutumia mashine ya mionzi yaliyokuwa yakitolewa leo kwa wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Fuwai iliyopo Beijing China Prof. Xiangbin Pan akimpatia zawadi kutoka china Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge baada ya mafunzo ya jinsi ya kuziba matundu na kuzibua mishipa ya damu ya moyo iliyoziba bila kutumia mashine ya mionzi kwa wataalamu wa JKCI leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi wa wataalamu wa afya kutoka Hospitali ya Fuwai iliyopo Beijing China na wenzao wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakisikiliza wakati wa mafunzo ya jinsi ya kuziba matundu na kuzibua mishipa ya damu ya moyo iliyoziba bila kutumia mashine ya mionzi leo katika taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwa katika picha ya pamoja na Wataalamu wa afya kutoka Hospitali ya Fuwai iliyopo Beijing China na wengine wa JKCI mara baada ya mafunzo ya jinsi ya kuziba matundu na kuzibua mishipa ya damu ya moyo iliyoziba bila kutumia mashine ya mionzi leo katika taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Picha na: JKCI