Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali Mkoa wa Songwe wamepatiwa elimu kuhusu saikolojia ya afya ya akili ikiwa ni pamoja na kubainisha faida ya afya ya akili katika majukumu yao ya kila siku na uwezo wa kukabiliana na msongo wa mawazo ili kuwa na ustawi bora sehemu ya kazi na katika familia.
Elimu hiyo imetolewa katika ukumbi wa Polisi uliyopo Vwawa Wilaya ya Mbozi Januari 15, 2025 na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Polycarp Urio kutoka Makao Makuu ya Polisi Dodoma akiambatana na Mwanasaikolojia wa afya ya akili Konstebo Omary Mbwegu.
SACP Urio amewataka askari hao endapo watapata msongo wa mawazo ni vyema kutafuta msaada wa haraka ili kuweza kutatua changamoto hiyo ya afya ya akili kabla hayajatokea madhara makubwa katika majukumu yao na kwa familia.
Afisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Songwe ACP Akama Shaaban