Happy Lazaro,Arusha .
WAZIRI wa Fedha Mwigulu Nchemba ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania{TRA} kuacha kuwahurumia na kuwa wakali kwa wafanyabiashara sugu wanaokwepa kulipa kodi ya serikali kwa makusudi bila kubugudhi biashara zao.
Nchemba ameyasema hayo Jijini Arusha wakati akifungua Mkutano wa watendaji wakuu wa TRA Nchini mkutano uliohudhuriwa na Wakuu wa idara ,Wakurugenzi TRA Makao Makuu ,Meneja TRA kutoka Mikoa ya Kikodi 33 Nchini na Wakuu wa TRA Wilaya zote nchini wakizungumzia utendaji na changamoto katika mwaka ulipita na kuweka mkakati wa utendaji kazi katika kipindi kijacho.
Amesema hakuna nchi Duniani iliyoendelea ambayo wafanyabiashara na wananchi hawalipi kodi hivyo aliwataka watumsihi wa TRA nchini kuacha huruma na kuwa wakali kwani mfanyabiashara na mwananchi asiyelipa kodi hapaswi kuheshimiwa.
Waziri amesema na kuwasihi watumishi wa TRA pamoja na kufanya kazi nzuri katika ukusanyaji mapato lakini hawapaswi kutengeneza Taifa la baadhi ya watu na wafanyabiashara kulipa kodi na wengine wasilipe hilo halipaswi kufanywa katika awamu hii ya Rais Samia Suluhu Hassan na hakuna Taifa lililoendelea ambalo wananchi wake na wafanyabiashara hawalipi kodi.
Akizungumzia baadhi ya wafanyabiashara kuwa na mashine ya EFD na wengine kutokuwa nayo huku wote wakifanya biashara zinazofanana alimtaka Kamishina wa TRA nchini kuliangalia hilo kwani linajenga matabaka pasipokuwa na sababu za msingi.
Waziri Nchemba amesema wafanyabiashara wote wenye sifa za kuwa na machine ya kukusanya kodi za EFD wote wanapaswa kufungiwa mashine hizo lengo ni kuondoa matabaka na madaraja yasiyokuwa ya msingi kwani kila mmoja anastahili kulipa kodi kwa kutumia mashine hizo.
Naye Kamishina wa TRA Nchini,Yusuph Mwenda amewashukuru walipa kodi nchini kwa kuwa wazalendo kwa kulipa kodi stahiki na kusema kuwa wadaiwa sugu wanapangiwa mpango kazi usiokuwa na bugudha ili waweze kulipa kodi stahiki.
Aidha amemshukuru Rais kwa kuhamashisha ulipwaji kodi kwa kutoa miongozi na kuhamashisha wafanyabiashara kulipas kodi kwani maendeleo hayawezi kuwepo iwapo wafanyabiashara na wananchi watashindwa kulipa kodi.
Amesema katika changamoto za wafanyakazi wa TRA wasikuwa waamini hatua kali zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na baadhi kufukuzwa kazi,kutelemshwa vyeo,kukatwa mishahara ikiwa ni njia pekee ya kuboresha utendaji kazi usikuwa na rushwa wala kufanya kazi kinyume na taratibu.
Naye Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu,Moshi Kbangwe amesema kuwa dhumuni la Mkutano huo ni kuangalia utendaji kazi wa mwaka uliopita na kutatua changamoto zake na kupanga mpango kazi wenye tija kwa ajili ya ukusanyaji mapato mwaka 2025.