SERIKALI imepeleka gari mpya ya wagonjwa kituo cha afya Ihalula kilichopo kata ya Utalingolo halmashauri ya mji wa Njombe ili kuwanusuru wagonjwa kutumia vyombo visivyo rafiki kwa usafiri vinavyoweza kuhatarisha usalama wao.
Katika Hafla ya Makabidhiano ya gari la wagonjwa wa Dharura Ambulance kwenye kituo Cha Afya Ihalula Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Deodatus Mwanyika amesema gari hilo limegharimu zaidi ya mil 250 hivyo kila mwananchi anajukumu la kulilinda na kulitunza ili kunufaisha vizazi vijavyo
Mbunge mwanyika amesema ujio wa gari hilo ni sehemu tu ya mengi mazuri yaliyofanywa na serikali katika sekta ya afya ikiwa ni pamoja ujenzi wa vituo vya afya,zahanati ,hospitali na dawa ili wananchi wapate huduma bora za afya.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Utalingolo Erasto Mpete Ambaye ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe ametumia fursa hiyo kuhamasisha watu kuzaliana ili kujaza mkoa wa Njombe wenye idadi ndogo ya watu kwasababu serikali ya awamu 6 imeendelea kuboresha huduma za afya nchini..
Awali mganga mfawidhi wa kituo Cha Afya Ihalula Dokta Happiness Kwilasa amesema ujio wa gari Hilo utasaidia kupunguza adha kwa wananchi ambao Wamekuwa wakitumia gharama kubwa kusafirisha wagonjwa pindi wanapopewa Rufaa.
Aidha Dokta Kwilasa amesema pamoja na ujio wa gari Hilo lakini Bado kituo kinakabiliwa na Changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa wataalamu na miundombinu hasa nyumba za kuishi.
Naye Dokta Jabil Juma mganga mkuu wa Halmashauri ya mji wa Njombe amesisitiza kutolewa Bure kwa huduma ya gari Hilo kwani ni jukumu la Serikali kugharamia huku akisema Tayari Magari matano yameshatolewa na yanafanyakazi.
Agnes Mbilinyi na Sebastian Fungilwa ni wakazi wa Ihalula kunako kituo Cha Afya ambao wanasema sasa watapata nafuu pindi wanapopatwa na Rufaa.
Diwani wa Kata ya Makowo Honolatus Mgaya anasema Kituo chake Cha Afya Makowo kilipata gari yapata mwaka Sasa lakini uendeshaji wake unategemea mapato ya ndani.
Kwa mujibu wa Mganga mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Njombe hadi sasa Halmashauri imepata magari matano ya Wagonjwa wa Dharura kwenye vituo vya Afya Vinne na Moja la Hospitali.