Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally atakuwa na ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Kigoma kuanzia tarehe 17 – 19 Januari, 2020.
Leo tarehe 17 Januari, Katibu Mkuu anatarajiwa kuwasili Uwanja wa ndege Kigoma Mjini kuelekea moja kwa moja wilayani Uvinza kata ya Kazuramimba ambapo atazungumza na wajumbe wote wa mkutano Mkuu wilaya ya Uvinza, Wazee, mabalozi, viongozi wa kata na matawi pamoja na mabaraza ya jumuiya zote wilayani hapo.
Kesho tarehe 18 Januari, Katibu Mkuu atakuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu maalum wa kupokea taarifa ya kazi za Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini wilayani Kigoma.
Atamalizia kwa kikao cha mabalozi wote wilaya ya Kigoma kesho kutwa tarehe 19 Januari, ambapo Katibu Mkuu atagawa vitambulisho kwa mabalozi wa wilaya hiyo ikiwa ni mfano kwa mabalozi wote nchini.