Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa azindua kliniki ya Biashara Zanzibar. Tukio hili lilishuhudiwa na Waziri wa Biashara na Viwanda Mhe Balozi Amina Salum Ali. Huduma ya Kliniki ya Biashara inalenga kutatua changamoto za biashara kwa wafanyabiashara kwa kuwahudumia ana kwa ana. Huduma hii hujumuisha taasisi zote za kimkakati katika kusaidia mnyororo wa biashara. Huduma ya Kliniki ya Biashara ilianzishwa na inasimamiwa na TanTrade
Watendaji kutoka taasisi mbalimbali za serikali ambazo ni wezeshi katika mnyororo mzima wa thamani ya biashara wakitoa huduma ya kusikiliza changamoto za wafanyabaishara Zanzibar kupitia huduma ya kliniki ya biashara inayoratibiwa na TanTrade
Katibu wa kampuni ya ZASCI Bw Rajah Lee akimuonesha Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TanTrade Dkt Ng’wanza Kamata zao la Mwani uliothirika na ukungu katika eneo la Glacilaria-Zanzibar. Kampuni ya ZASCI ni miongoni mwa makampuni yanayozalisha na kuuza bidhaa ya zao la mwani-Zanzibar na TanTrade imekuwa na jukumu la kutoa mafunzo kwa wazalishaji wa zao hilo katika kuongeza thamani zao hilo na kulitafutia masoko ya nje.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TanTrade akiangalia zao la mwani na kusaidia kuvuna mwani aina ya Cottonue pamoja na wakulima wa Mwani katika eneo la Bweleo Magharibi ya Unguja. Lengo la kufanya ziara katika eneo la uzalishaji wa Zao la Mwani ni kufahamu maendeleo ya uzalishaji wa zao la mwani.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi Latifa Khamis akimpa maelezo Mhe Innocent Bashungwa Waziri wa Viwanda na Biashara namna Huduma ya Kliniki ya Biashara itakavyofanya kazi Zanzibar ili kutatua changamoto mbalimbali za wafanyabiashara.