MBUNGE wa Magu (CCM),Boniventura Kiswaga amesema sh. bilioni 143.9 zilizotolewa na serikali katika kipindi cha 2020 hadi 2024,zimemeleta mageuzi makubwa ya maendeleo na kubadilisha maisha ya wananchi wa Wilaya ya Magu.
Amesema hayo leo,mjini Magu wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika Mkutano Mkuu wa CCM Jimbo la Magu ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.Dkt. Doto Biteko.
“Fedha hizo sh. bilioni 143.9 zimetekeleza miradi ya maendeleo, nimefanya kazi kwa karibu na jamii kwa miaka minne nikipita kila kijiji kueleza mafanikio ya serikali ya awamu ya sita na wananchi wanayafahamu,hivyo Jimbo la Magu limetekeleza kwa vitendo ilani ya uchaguzi na kuleta matokeo chanya kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo,”amesema Kiswaga.
Amesema kuwa Mfuko wa Jimbo,ulitumia sh. milioni 336.7 kuchochea miradi ya maendeleo 52 kati ya hiyo ya afya 28, elimu 20,mitatu ya utawala na mmoja wa barabara huku sh.milioni 78 zikitumika kwa ujenzi wa barabara na madaraja.
Pia,sh.bilioni 7.1 zilipolekelewa na TARURA ili kuhudumia barabara za vijijini za urefu wa km 1,524.15 zilizoshindikana kutengenezwa huku Rais Dk.Samia Suluhu Hassan akileta sh.milioni 830 kabla ya kuongeza sh. bilioni 1.5 na hivyo kufikisha jumla ya sh.bilioni 2.3 za barabara na kuweza kuunganisha kijiji na kijiji.
Kiswaga amesema serikali ya aamu ya sita inajenga barabara ya Magu-Jojiro Kwimba ya urefu wa km 64 kwa kiwango cha lami,inajenga Daraja la Mto Simiyu kwa sh.bilioni 48,pamoja daraja la Ndagalu na Itumbili linalogharimu sh.bilioni 9.4.
Mbunge huyo wa Magu amesema katika kipindi cha maka 2020 hadi 2024, sh. bilioni 12.1 zilitumika kutekeleza miradi ya maji ambapo baada ya kukamilika kwa mradi wa maji Magu mjini idadi ya watumiaji imeongezeka, mradi unahudumia watu 68,694 kati ya 73,600 wa kata za Itumbili, Magu mjini, Isandula, Kandawe, Nyigogo na baadhi ya Kata ya Kahangara.
Aidha,unajengwa mradi mkubwa wa maji unaojengwa kwa gharama ya sh.bilioni 3.5,utakuwa mwarobaini wa changamoto hiyo katika kata za Bujora,Kisesa na Bukandwe, tayari serikali imekamilisha chanzo cha Butimba,ujenzi wa tenki la ujazo a lita milioni tano umefikia asilimia 92.
Kiswaga alisema kwa upande wa vijijini RUWASA imekamilisha miradi 18 ya maji kwa sh. bilioni 8.3 ambapo idadi ya watumiaji wa maji ya bomba imeongezeka kutoka asilimia 56 mwaka 2020 hadi asilimia 75 mwaka 2024.
“Miradi ya Sagani-Mwamabanza,Iseni-Nnyang’hanga,Misungwi- Lumeji,inaendelea kutekelezwa na itakapokamilika itapunguza uhaba wa maji wa majisafi na salama kwa kiwango kikubwa vijijini,”amesema.
Kwa mujibu wa Kiswaga,sekta ya usafiri wa majini serikali inakamilisha kivuko cha Ijinga-Kahangara kilichogharimu sh.bilioni 5.3, ambaho kitafungua fursa za kiuchumi ka wakazi wa kisiwa cha Ijinga,miumbombinu hiyo inadhirisha kukua kwa Magu kiuchumi,mawasiliano na biashara.
Amesema mafanikio mengine ya kujivunia ni ya sekta ya elimu ambapo sh.bilioni 31.1 za miradi ya elimu ya awali,msingi, sekondari na vyuo vya ufundi ambapo kinajenga chuo cha VETA huko Nsola kwa bilioni 1.6.
Pia,katika mwaka 2021 hadi 2024,halmashauri ilitekeleza ujenzi miundombinu ya madarasa ya shule za msingi,nyumba za walimu, matundu ya vyoo na shule tano mpya ikiwemo Chifu Hangaya kwa sh.bilioni 7.3 huku miradi 19 ya elimu ya sekondari ikigharimu sh.bilioni 21.5.
“Kwangu mimi Mungu amekuwa tegemeo langu kwa kila kitu na kuniwezesha kutekeleza mipango ya maendeleo ya wananchi jimbo la Magu.
“Namshukuru Rais Dk.Samia,kwa hekima,busara,subira na unyenyekevu,ameidhirishia dunia kuwa ni kiongozi mchakapakazi mwenye shauku ya kujenga nchi yake,Mzalendo, mkombozi wa Watanzania,mwanademokrasia aliyejipambanua Afrika na Duniani kwa kudumisha umoja,amani na mshikamano,”amesema Kiswaga.