MBUNGE wa Nyamagana (CCM), Stanslaus Mabula,amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi katika kipindi cha miaka minne (2020-2024) akijivumia utekelezaji kwa kiwango.
Pia,amemshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,kwa kutoa fedha zaidi ya sh.bilioni 402 za miradi ya maendeleo jimboni humo.
Mabula aliwasilisha taarifa hiyo leo,katika Mkutano Mkuu wa CCM Jimbo la Nyamagana,uliohudhuriwa na wajumbe 666 kati ya 750 ambpo mgeni ramsi alikuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda.
Amesema,katika kipindi cha miaka minne miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za afya,elimu,maji na barabara,imetekelezwa kkwa kiwango cha hali ya juu a,bapo viyuo vya afya na zahanati 97 zimejengwa vikiwemo vya sekta binafsi.
Amesema sekta ya elimu hadi kufikia Novemba 30,mwaka huu,zaidi ya sh.bilioni 29.6 za elimu bila malipo zilipokelewa,shule za msingi nane zenye thamni ya zaidi ya sh.bilioni 2.7 zimejengwa na sekondari nne kwa sh.bilioni 2.03.
“Kipekee namshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za maendeleo katika Jimbo la Nyamagana ili kuboresho sekta zinazowagusa wananchi moja kwa moja,kati ya sh.Trilioni 5.6, Nyamagana tulipata zaidi ya bilioni 400,”amesema Mabula.
Amesema jimbo la Nyamagana lilipata sh.bilioni 402 kati ya sh.trilioni 5.6 za miradi ya maendeleo iliyosimamiwa kwa ushirikiano wa serikali,mbunge na madiwani na maendeleo hayo yanaonekana kwa macho.
Mabula amesema,Jimbo la Nyamagama lilipata sh.bilioni 1.8 kati ya bilioni 3 za miradi ya BBT,zilizoelekezwa katika sekta ya uvuvi ambapo vijana walinufaika kwa kufanya ufugaji wa samaki kwa vizimba huku jiji likitenga sh.milioni 500 za kuwaongezea nguvu.
Amesema kwa miaka mitatu na nusu,Jiji la Mwanza (Nyamagana),maji kilikuwa kilio kikubwa na miundombinu ya barabara,hivyo serikali imejenga chanzo kipya cha maji Butimba ili kuwaondolea wananchi kadhia hiyo.
“Mradi wa maji Butimba umekuwa mkombozi lakini tumeongezwa sh.bilioni 49 za kujenga matenki ya kuhifadhi maji huko Sahwa,Mkolani na Fumagila,hivuo ifikapo Januari mwakani,ndoto ya Nyamagana kuondokana na adha ya maji tutakuwa tumepiga hatua,”ameeleza Mabula.
Kuhusu miundombinu Mbunge huyo wa Nyamagana alisema,kuna km 1,020 za barabara zinazopitika si zaidi ya asilimia 35,lakini katika uongozi wa Rais Dk.Samia,TARURA imepata sh.bilioni 20 za kusaidia ujenzi wa barabara za pembezoni kwa kutumia zege na mawe yakiwemo madaraja madogo madogo.
“Barabara Kuu ya Kenyatta-Shinyanga,itajengwa kwa njia nne kuanzia Igogo hadi Usagara baada ya zaubini kutangazwa.Madaraja ya Mabatini na Mkuyuni yamekuwa yakisababisha maafa,sh.bilioni 11 zimepatikana, sh.bilioni 5zitaumika kujenga daraja la Mkuyuni na Mabataini sh.bilioni 6,”alifafanua Mabula.
Aidha,ameeleza kuwa sh.bilioni 10 zilishatengwa za ujenzi wa barabara ya Mkuyuni,Tambukareli,Mahina hadi Mwatex kwa kiwango cha lami,lakini bado mkandarasi hajapatikana.