Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 20, 2024 ameongoza wageni mbalimbali katika uzinduzi wa Tuzo za Uhifadhi na Utalii zinazofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Mt. Meru Arusha ambapo pia anazindua tuzo hizo
Tuzo hizo zitasaidia kuchochea ushindani mzuri kati ya wadau wa sekta ya maliasili na utalii na hatimaye kuwezesha kuboresha utoaji huduma, kuhifadhi mazingira hivyo kuchangia katika kukuza sekta.
Wageni mbalimbali tayari wamewasili katika Hoteli ya Mt. Meru Arusha kushuhudia tukio la kihistoria la Uzinduzi wa Tuzo za Uhifadhi na Utalii leo Disemba 20, 2024.