VICTOR MASANGU, PWANI
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani imesema kwamba itawahudumia walipakodi wake kwa kuzingatia misingi imara ya kuwa na uadilifu, uwajibukaji,, weledi pamoja na suala la kuwa na uaminifu pamoja na kuweka mikakati endelevu ya kuwatembelea sehemu zao za biashara kutoa ushauri, kusikiliza changamoto zinazowakabili.
Hayo yamebainishwa na Kamishina wa uchunguzi upande wa Kodi Hashimu Ngoda wakati wa kikao na na baadhi ya viongozi wa jumuiya za wafanyabiashara, viongozi wa dini, pamoja na watendaji wa TRA kwa lengo kuweza kubadilishana mawazo,kusikiliza changamoto, kupeana ushauri ambao utaweza kusaidia katika kuongeza kasi ya ukusanyaji wa kodi.
Ngoda amebainisha kwamba TRA kwa sasa wapo katika mwezi wa hamasa hivyo wameamua kufanya ziara katika maeneo mbali mbali kwa lengo la kukutana na walipakodi wao ikiwa sambamba na kutoa ushauri,kusikiliza changamoto zinazowakabili na kuweka mikakati ya pamoja ambayo itaweza kusaidia katika ukusanyaji wa kodi.
“Mkoa wa Pwani ni moja kati ya Mkoa muhimu sana katika ukusanyaji wa mapato kwani katika kipindi cha miezi mitano wameweza kufuka malengo ambayo wamejiwekea katika ukusanyaji na ukizingatia kwa sasa TRA tupo katika mwezi wa hamasa ndio maana tumeamua kuwatembelea walipa kodi wetu na kuwapongeza kwa kutoa kodi kwa hiari,”alisema Meneja Masawa.
Naye Meneja wa TRA Mkoa wa Pwani Masawa Masatu amewashukuru kwa dhati wafanyabiashara wote wa Mkoa wa Pwani na kuwaomba wanaendelee kushirikiano kwa hali na mali katika suala zima la ulipaji wa kodi kwa hiari ili serikali iweze kukusanya mapato yake kwa maendeleo ya wananchi.
Napendakuchukua fursa hii ya kuwapongeza kwa dhati wafanyabiashara wote wote ndani ya Mkoa wa Pwani na kitu kikubwa ninawashauri kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa katika kulipa kodi na lengo letu ni kukusanya mapato mengine ambayo yatasaidia kupata fedha na serikali kuweza kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo,”alibainisha Meneja Masawa.
Nao baadhi ya viongozi wa dini akiwemo Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Pwani Hamisi Mtupa ameipongeza TRA kwa kuweza kuweka mazingira mazuri kwa wafanyabiasshara tofauti na kipindi cha miaka ya nyuma na kuwahimiza wahakikishe wanaendelea kulipa kodi kwa hiari kwa maslahi ya wananchi.
Wafanyabiashara amabao wameshiriki katika kikao hicho wamesema kwamba TRA Mkoa wa Pwani kwa sasa imekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu na mafunzo mbali mbali ambayo yameweza kuwasaidia katika kuendesha shughuli zao za kibiasshara bila kupata usumbufu wa aina yoyote ile.
Ziara ya mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani inaendelea kufanya ziara katika maeneo mbali mbali kwa ajili ya kuwatembelea walipa kodi wao ikiwa ni mwezi wa hamasa wenye lengo la kuweza kutoa elimu,ushauri, pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili ili kuzitafutia ufumbuzi katika suala zima la kulipa kodi kwa hiari kwa maendeleo ya Taifa.