Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela amekipongeza chuo cha usimamizi wa fedha (IFM), kwa kuongeza masomo ya kufundisha kutoka mpaka kufikia zaidi 39 tofauti na ilivyokuwa kipindi wanasoma ambapo yalikuwa mawili na kudai kuwa hayo ni maendeleo makubwa kwa chuo hicho.
Bw. Nsekela amayasema hayo Jijini Dodoma kwenye hafla ya Chakula cha jioni cha mkutano wa wanachuo waliomaliza IFM (The IFM alumni reunion dinner), huku akiongeza kuwa wao kama wahitimu wanayo nafasi ya kujivunia kuwa sehemu ya chuo hicho.
“Lakini niwapongeze kwa kuongeza matawi ya chuo chenu kwasababu itasaidia kupata wanafunzi wengi kuja kusoma kwenye chuo chenu pamoja na kufanya wanafunzi wengi watamani kuja kusoma hapa hilo nalo ni jambo jema niwapongeze sana,”amesema.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha IFM Prof. Joseph Lotto amewaomba wanachama hao kuwaunga mkono pale wanapokuwa wanajitafuta kupata nafasi kwa wanafunzi wanaofanya mafunzo kwa vitendo kuwapatia nafasi kwenye ofisi zao ili wawe na uwezo wa kuajirika na kuweza kuwa na mchango kwenye sokola ajira.
“Kwa siku za hivi karibuni wanafunzi wetu wanapofika kwenye maofisi yenu asilimia kubwa ya wanafunzi wetu naishia kukoroga chai na kutumwa kubeba mafaili, mwisho wa siku baada ya miezi mitatu wanarudi kama walivyokwenda na hawajapata kile kilichokusudiwa katika ile miezi mitatu,”amesema.
Amesema wao kama wadau wa maendeleo wa IFM kama wakiamua kuwasaidia watawasaidia kupata kupata ujuzi unaotakiwa na kuongeza kuwa wataenda kutengeneza mfumo ambao utawasaidia waajiri kupata kazi za wanafunzi wa chuo hicho wanazozifanya ili kuwasaidia kupata nafasi na waajiri kujionea kile wanachokifanya.
Pia amesema kuwa kwasasa chuo hicho kinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa miundombinu ya madarasa na mabweni, uhitaji wa mitaala inayokidhi mahitaji wa soko la ajira kwa wanafunzi na uhitaji rasilimali watu wenye ujuzi kuweza kutoa huduma kwa ufasi.
“Chuo kinaendelea kubuni njia ya kutatua changamoto hizo huku tukizingatia mabadiliko ya kisera na mahitaji ya kitaifa na chuo chetu pia kimebuni utaratibu wa kuunga mkono juhudi za serikali za kuinua elimu rasmi kwa kuwajengea uelewa na kuwapa motisha wanafunzi na wazazi ambapo hili linatokana na uzoefu wetu tulio nao wa zaidi ya miaka 10 huko kanda yaziwa na hili niliweke wazi kuwa tumekuwa tukishirikiana na jamii zilizo nyuma kielimu,”amesema.
Katika hafla hiyo jumla ya kiasi cha fedha Milioni 44 zilichangwa ambapo ahadi ni Milioni 36 na pesa taslimu ni Milioni 8.