Na Neema Mtuka Sumbawanga
Rukwa .Halmashauri ya wilaya Nkasi mkoani Rukwa imetoa ufafanuzi juu ya tukio la Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Izinga tarafa ya Wapembe Legiucy Martin Kawimbe anayedaiwa kuwafukuza shule Wanafunzi 9 kuwa hayakuwa maelekezo ya Serikali.
Akitolea ufafuzi Leo Dec 5 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi wa Halmashauri ya Nkasi Afrah Hassan amesema chanzo kilikuwa ni mgogoro kati ya walimu na wazazi uliojitokeza Kijijini hapo uliopekekea mwalimu mkuu kuwa simamisha shule na kuwataka wazazi wawatafutie wanafunzi hao shule nyingine.
Hassan amesema mwalimu huyo kwa kufanya hivyo alienda kinyume na utaratibu na wanafunzi hao tayari wamerejeshwa shuleni na hatua za kinidhamu zitachukuliwa pindi uchunguzi unaendelea utakapokamilika.
“Mapema Leo Kuna taarifa iliyokuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii juu ya mwalimu mkuu wa shule ya Izinga iliyopo Wampembe wilayani Nkasi kuwafukuza wanafunzi 9 kama ni maelekezo ya Serikali na baada ya kufuatilia kwa kina suala hilo tumebaini kuwa Mwalimu huyo aliwasimamisha shule wanafunzi hao baada ya kutoelewana na wazazi”. Alifafanua Mkurugenzi
Aliongeza kuwa hatua za haraka zilizochukuliwa ni kuwarejesha shule wanafunzi hao bila ya masharti yoyote kwani hatua alizozichukua mwalimu mkuu wa shule hiyo ni kinyume na utaratibu na tayari wameanzisha uchunguzi wa suala hilo.
“Kama ikibainika kutenda kosa hilo hatua stahiki za kinidhamu na uongozi zitachukuliwa kwani kama mgogoro unawahusisha wazazi na walimu wanafunzi hawahusiki kwa lolote”.
Mkurugenzi Mtendaji huyo alidai kuwa katika taarifa iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kuwa maelekezo ya kuwafukuza watoto hao yalitolewa na wizara ya elimu kupitia kwa mkuu wa wilaya ya Nkasi hayana ukweli wowote.
Aidha ameitaka Jamii kuacha tabia ya kusambaza taarifa ambazo hazina ukweli kwani wanafunzi hao walisimamishwa kwa sababu wazazi wao walihitilafiana na walimu Ambapo wazazi hao waliwarushia walimu lugha za matusi na ndipo mkuu wa shule akachukua uamuzi wa kuwasimanisha wanafunzi hao na kutaka wahamishiwe shule nyingine.
Alisisitiza kuwa uamuzi wa mkuu huyo wa shule haukufuata utaratibu wa kisheria na ndiyo maana wakatoa amri ya wanafunzi hao kurejeshwa shuleni mara Moja.
Alidai kuwa hatua zilizochukuliwa za haraka ni kuwarejesha shule Watoto hao bila ya masharti yote kwani hatua alizozichukua Mwalimu mkuu wa shule hiyo ni kinyume na utaratibu wa kisheria.
Sambamba na hilo alisema kuwa serikali itahakikisha Wanafunzi wa shule hiyo na shule nyingine katika Halmashauri ya wilaya Nkasi watasoma bila kubughudhiwa Wala kuingizwa katika migogoro yoyote ya kijamii na kisiasa.
Wanafunzi hao waliorejeshwa shule katika shule hiyo ni Mathias Sweet beth Kabezya wa darasa la (|||),Anakreda Sweet beth Kabezya (|),Grace Boniface Kabezya (lV) Antonio Boniface Kabezya (lV),Venus Boniface Kabezya ((ll) na Clephace Adabeth Kabezya (lV)
Wengine ni Lilian Sweet beth Kaswanya (V), Rosemary Sweetbeth Kaswanya (lll) na Joseph Sweetbeth Kaswanya (Il