Na Silvia Mchuruza.
Kagera.
Zaidi ya Miradi mbalimbali ya kimaendeleo imeendelea kutekelezwa katika kata ya Ruzinga iliyopo Wilayani Missenyi Mkoani Kagera ikiwa ni kuazimisha miaka 14 ya uchangiaji maendeleo katika kata hiyo.
Miradi hiyo ni kama bweni la kulala wanafunzi, vyumba vya mahabara,ukarabati wa madarasa, mfumo wa computa, sekta ya maji pamoja na afya.
Hayo yamebainishwa na Kaimu mwenyekiti wa tamasha hilo linalofahamika kama Ruzinga Development {Ruzinga day} bwana Paschael Kamala wakati akiongea na halaiki ya watu waliofika kwa lengo la kushuhudia tamashahilo.
Bwana Kamala ameongeza kuwa zaidi ya shilingi milioni 20 zimechangwa katika tamasha la kila mwaka kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya Kata Ruzinga iliyopo Wilayani Missenyi Mkoani Kagera.
Bwana Kamala amesema kuwa pesa hizo zitatumika kwa ajili ya kuendelea kuchochea maendeleo ya kata ikiwemo miundombinu ya barabara, maji, elimu, pamoja na afya uku akiendelea kuomba msaada katika halmashauri ya Wilaya ya Missenyi na Tanzania kwa ujumla kuunga mkono jitihada za wadau hao ambao wana uchu wa kuona kata hiyo inapiga hatua kubwa kwenye sekta ya maendeleo .
Pamoja na michango hiyo wadau mbali mbali wa Ruzinga day wametembelea miradi kadhaa ili kujionea hali halisi ikiwemo kukagua shule ya sekondari Ruzinga,kituo cha afya Ruzinga pamoja na shule ya msingi Ruhija huku wadau hao wakishuhudia uchakavu mkubwa wa baadhi ya majengo ya shule ya msingi Ruhija ambapo wameomba uongozi wa wilaya ya Missenyi kushirikiana nao kufanya marekebisho.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika tamasha hilo ambaye ni mkurugenzi wa harmashauri ya wilaya ya Missenyi bwana Innosent Mkandala amesifu juhudi kubwa zinazofanywa na wadau hao wa maendeleo katika kata hiyo na kueleza kuwa serikali itaendelea kushirikiana nao huku akiwaasa wazazi kuhakikisha wanawapelea shule wanafunzi waliochaguliwa kijiunga na kidato cha kwanza mwaka huu.
Katika hatua nyingine bwana Mkandara amewapongeza wadau hao wa maendeleo katika kata hiyo kwa kuonesha jitihada kubwa za kuinua maendeleo ya kata hiyo huku akitaja bweni la kulala wanafunzi wa kike ambalo limejengwa kwa jitihada kubwa za wadau hao wa maendeleo pamoja na serikali na kusema kuwa kata hiyo ya Ruzinga ni moja kati ya kata zinazozidi kupiga hatua kubwa za kimaendeleo na kuwa mfano wa kuigwa Wilayani Missenyi.
Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo Mh Leonidas Rutagwelela ameipongeza halmashauri ya Wilaya ya Missenyi kwa misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikipelekwa katika kata hiyo pindi wanapoitaji msaada wa halmashauri hiyo na kuongeza kuwa wamekuwa wakiwa unga mkono mara kwa mara.