Mwanasheria Mkuu wa Serikali Hamza Johari akizungum na Waandishi wa habari kuhusu kikao kazi na Wakurugenzi wa idara na wakuu wa vitengo vya huduma za sheria Serikalini kinacho tarajiwa kufanyika kesho Disemba 6,2024 katika ukumbi wa mikutano wa Jiji la Dodoma.
…………….
Na Gideon Gregory, Dodoma.
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeandaa kikao kazi na Wakurugenzi wa idara na wakuu wa vitengo vya huduma za sheria Serikalini kinacho tarajiwa kufanyika kesho Disemba 6,2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliopo katika mji wa Kiserikali Mtumba.
Hayo yamebainishwa leo Disemba 5,2024 Jijini Dodoma na Mwanasheria Mkuu Mh. Hamza Johari wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuelekea katika kikao hicho ambapo pamoja na mambo mengine atatoa maono yake (Vision) kwenye sekta ya sheria nchini.
“Ili kuzikumbusha Wizara, Taasisi, Idara, Vitengo pamoja na Mawakili wa serikali wanaotekeleza majukumu ya ofisi yangu, nimeona ni muhimu kuandaa kikao kazi ambacho litafanyika kesho Disemba 6,2024 na lengo la kikao kazi hicho ni kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji katika utoaji huduma za sheria Serikalini, “amesema Mhe. Hamza.
Amesema kupitia kikao hicho mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi huku wakikumbushana umuhimu wa kuzingatia sheria, taratibu, mipango ya maendeleo, dira na miongozo mbalimbali ya serikali watakayo paswa kuzingatia wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.
“Ni matarajio yangu kwamba kikao hicho kitazaa matunda mema kwani naamini kitatoa uelekeo na mikakati ya kutoa huduma bora za sheria Serikalini, kwani mawakili wa serikali ni jeshi ambalo linalinda uchumi wa nchi kwa kutumia kalamu,”amesema.
Pia ameongeza kuwa anaamini maelekezo ya serikali atakayoyatoa kupitia kikao hicho muhimu yatatekelezwa ili kuleta maendeleo kwa wananchi.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Hamza Johari akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu kikao kazi na Wakurugenzi wa idara na wakuu wa vitengo vya huduma za sheria Serikalini kinacho tarajiwa kufanyika kesho Disemba 6,2024 katika ukumbi wa mikutano wa Jiji la Dodoma.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza Johari akizungumza na Waandishi wa habari, kulia kwake ni Bi. Neema Ringo Kaimu Mkurugenzi wa utafiti na huduma za ushauri wa Kisheria kuhusu kikao kazi na Wakurugenzi wa idara na wakuu wa vitengo vya huduma za sheria Serikalini kinacho tarajiwa kufanyika kesho Disemba 6,2024 katika ukumbi wa mikutano wa Jiji la Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali waliohudhuri katika mkutano wa mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza Johari wakati akizungumza na Waandishi wa habari.